Monday 30 June 2014

KAGASHEKI CUP 2014: TIMU YA KAGONDO YAITUNGUA BUHEMBE FC BAO 1-0

Na Faustine Ruta, Bukoba.
Timu ya Kagondo FC imejipatia Alama tatu muhimu kwenye Mtanange wao dhidi ya timu ya Buhembe FC leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwenye Michuano ya Kombe la Kagasheki. Bao hilo la pekee lilifungwa na Mchezaji namba tisa Mgongoni Abduratif Khamis katika kipindi cha kwanza dakika 37. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili timu zote mbili hakuna iliyoziona nyavu za mwezake timu licha ya kushambuliana mara kwa mara. Mwamuzi alipuliza kipenga dakika 90 kumaliza mtanange huo na Timu ya Kagondo FC wakiibuka na ushindi huo wa bao 1-0. Mapema leo Mchana Timu ya Nshambya na Kibeta ziliumana na timu zote mbili zilimaliza mtanange kwa sare ya bila kufungana kwa kutoka 0-0. Kesho Ligi hii inaendelea tena kwa siku ya nne na kutakuwepo na michezo miwili, Mapema ni Nyanga vs Kitendaguro na Jioni saa 10:00 ni Wagonga Nyundo "Ijuganyondo Vs Kahororo".

Kikosi cha Timu ya Kagondo Fc
Kikosi cha Timu ya Buhembe FC
Timu Kapteni na waamuzi wakiteta kabla ya Mpambano hii leo kwenye uwanja wa Kaitaba,Bukoba Mjini

Kipute kilianza kwa Timu ya Buhembe kwa kasi sana
Kila Mtu na wake!
Patashika katikati ya uwanja
Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakishangilia bao lao lililofungwa na Abduratif Khamis katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza. kulia ni kipa wao nae alikuja kuwapongeza!!!
Mtanange ulikiendelea kipindi cha pili...
Frii kiki kuelekea kwenye lango la Kagondo FC
Mchezaji wa Kagondo aliumia, Watoa huduma ya kwanza wakimpa msaada wa kumtoa nje ya uwanja kwa matibabu
Lakini aliumia na kadi yake ya Njano ilimfata huko huko nje!

Kipa wa Kagodo chupuchupu afungwe bao hapa katika kipindi cha pili. Kipindi cha pili hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake bao hilo lilidumu mpaka dakika za mwisho

Hatari: Kipa wa Kagondo Fc akidaka mpira wa Kona

Kipindi cha Pili dakika za mwishoni Timu ya Buhembe FC ilipata kona mbili lakini haikuweza kusawazisha bao, licha ya kuliandama lango la wenzao Kagondo Fc.
Kipa akipangua mpira uliopigwa kwa kona..dakika za mwishoni.

No comments:

Post a Comment