Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipokea
Rasimu ya pili ya katiba mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba
mpya, Joseph Warioba, wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais, aliitaka Tume hiyo kuiweka Rasimu
hiyo kwenye mitandao ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza
kutoa maoni yao kwa urahisi kupitia mitandao.
Naye
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Warioba, alisema kuwa kulingana na idadi
ya kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali
tatu, alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu walihitaji Serikali tatu
kuliko walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa
itabaki ni kazi ya maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuungwa
mapema mwezi Januari mwakani.
Rais jakaya Kikwete, akimkabidhi raismu hiyo Makamu wake baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ta katiba mpya.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Risimu hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda na baadhi ya viongozi.
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa, waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya waasisi waliokabidhiwa Rasimu hiyo na Rais kikwete, baada ya kukabidhiwa.
Tundu Lissu, na wenzake wakiangua kicheko baada ya kutaniwa na Rais wakati akisoma hotuba yake kwenye hafla hiyo.
Zitto Kabwe, akiisoma Rasimu hiyo kwa makini.......
Jaji Warioba, akimkabidhi Rasimu hiyo, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Shein.
Rais akipokea Rasimu hiyo.....
Rais Jakaya Kikwete akihutubia baada ya kupokea Rasimu hiyo.
Eti na huyu jamaa naye alikuwa akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais kuhusu Rasimu hiyo...
Mtangazaji wa ITV na Redio One, Alfred Masako (kushoto) na Dkt. Kitila, wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais.
Sehemu ya wananchi na viongozi waliohudhuria hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Warioba, akizungumza.
Umakini wa kusikiliza....
Rais Jakaya akiteta jambo na Jaji Warioba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Prof. Ibrahim Lipumba.
Picha ya pamoja...... RASIMU YA KATIBA MPYA
No comments:
Post a Comment