Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest
Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa
iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla
ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu
alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal
Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha,
taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman
Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika
muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla
ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa
Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations). Mkuu wa Jeshi la
Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja
vya Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment