BARAZA
la Taifa la Usalama Barabarani limeanzimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani mikoa yote nchini Tanzania leo tarehe 23.09.2013 ambayo
yanatarajiwa kufika kikomo wiki ijayo tarehe 27.09.2013. Lengo kuu la
maadhimisho haya ni kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara
kwamakundi yote ya watumiaji wa Barabara.
Pamoja na kuwa
maadhimisho haya yatafanyika mikoa yote nchini kwa kupitia Kamati za
mikoa za usalama barabarani zilizopo kila mkoa, ambapo kitaifa
maadhimisho haya yanafanyika mkoani Mwanza.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Usalama Barabarani unaanzia kwangu, kwako na sisi sote ”
(Road safety starts with me, you and all of us)

Maandamano kulekea uwanja wa Kaitba Bukoba mjini.

Wanafunzi
wa shule ya kolping waliokuwa na shughuli ya kupiga tarumbeta wakati wa
sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama zilizofanyika
kwenye viwanja vya kaitaba leo hii Bukoba.

Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa kila mtumiaji barabara ana wajibu wa kuhakikisha Usalama Barabarani unaimarika.

Kuelekea Uwanjani Kaitaba...

Kuelekea Uwanjani Kaitaba ambako maadhimisho hayo yamefanyikia hii leo

Wanafunzi
kutoka Shule za Msingi nao walikuwepo kwa swala zima na kupata mafunzo
hayo na kupata elemu ya Usalama Baabarani kuzingatia kauli mbiu
ikisema.....
“Usalama Barabarani unaanzia kwangu, kwako na sisi sote ”

Wanafunzi wa shule ya kolping waliokuwa na shughuli ya kupiga tarumbeta
wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
zilizofanyika kwenye viwanja vya kaitaba leo hii Bukoba.

Wanafunzi wa shule ya kolping waliokuwa na shughuli ya kupiga tarumbeta
wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
zilizofanyika kwenye viwanja vya kaitaba

Wanafunzi wa shule ya kolping waliokuwa na shughuli ya kupiga tarumbeta
wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
zilizofanyika kwenye viwanja vya kaitaba leo hii Bukoba.

Wanafunzi wa shule ya kolping.

Waimbaji wa KAKAU Band kutoka hapa Bukoba wakiimba uwanjani Kaitaba hii leo

Kakau Band wakifanya yao uwanjani Kaitaba.

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akiingia Uwanjani na hapa akisalimiana na baadhi ya viongozi.

Kuelekea uwanja wa Kaitaba.

Dreva
Bw. Mbelwa (kushoto) nae alikuwepo uwanjani hapo kuhakikisha swala hili
la Usalama barabarani linaadhimishwa kwa kutoa elimu kwa wote!

Vijana wa Baodaboda wakitoa yaliyo moyoni mwao kwenye bango!!

Waimbaji wa Kakau Band wakiendelea kutumbuiza uwanjani hii leo

Kakau Band wakitumbuiza kwa nyimbo zao za kuhamasisha swala zima la Usalama Barabarani.
Wito
kwa abiria kutoshabikia vitendo vya ukiukwaji wa sheria kama vile
mwendokasi, abiriawanatakiwa kukemea na kutoa taarifa kwa Jeshi la
Polisi pindi waonapo ukiukwaji wa sheriana kanuni za usalama barabarani
wasisite kutuma taarifa hizi kupitia namba za simu zaviongozi wa Polisi
katika mikoa husika ambazo zimebandikwa kwenye baadhi ya mabasi.

Waimbaji wa Kikundi cha Kakau wakiimba hapa kwa furaha.

Bw.Winston
Kabantega Mkurugenzi wa CHUO cha Mafunzo ya Udereva cha Lake Zone
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kagera,
akizungumza na umati wa watu waliojitokeza uwanjani Kaitaba leo hii
mchana. Pia mkuu huyo amewasihi wapanda pikipiki kuacha tabia ya kupakia
abiria zaidi ya mmoja (mshikaki), kufuataalama na ishara zinazotolewa
na wasimamizi wa sheria, kuzingatia uvaaji wa kofia ngumu(helmet) na pia
kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi pindi wanapohusika katika
ajali.

Mkuu
wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe wa kwanza kulia toka
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho haya ya Wiki nenda kwa
usalama.

Baadhi ya viongozi wa serikali.
Pia
Viongozi wamewashauri madereva wote wa magari kujiepusha kuendesha
magari wakiwa wamechoka au wakiwa wametumia kilevi. Tunawahimiza
madereva na abiria kufunga mikanda ya usalama wawapo safarini, kwani kwa
kiasi kikubwa mikanda hii husaidia kupunguza vifo na ukubwa wa madhara
ya majerahakatika matukio ya ajali. Kabantega ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kagera, alisema chuo chake
kinafanya kazi ya kuwahamasisha madereva hao ili wajiunge na vyuo
vinavyotoa mafunzo ya udereva kwa kuwa vitawasaidia kufanya kazi zao kwa
ufanisi zaidi.

Kikosi cha zimamoto
No comments:
Post a Comment