Wednesday, 27 June 2018

NMB BUKOBA YAWAJENGA WATOTO KISAIKOLOGIA,KUJIWEKEA AKIBA BENKI.

 Katika kusherekea siku ya Baba duniani, Benki ya NMB  imeandaa hafla maalumu iliyokutanisha watoto wa shule za awali mpaka Darasa la saba, Hafla hiyo ilifanyika katika tawi la Bukoba. Mbali na mambo mengine watoto hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya benki na kufundishwa namna shughuli za kibenki zinavyofanyika,Watoto walipata zawadi mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya masomo yao shuleni, walijengwa kisaikologia kutambua umuhimu wa kufungua akaunti na namna ya kuweka akiba kwa ajili ya karo na matumizi yao,Pia walishiriki viburudisho mbalimbali na kukata keki kuashiria na kutambua siku ya Baba duniani.(KATIKA PICHA AFISA WA NMB AKIKATA KEKI NA WATOTO)


Watoto wakiulizwa maswali na Afisa wa benki baada ya  kufundishwa shughuli za benki.
 Watoto wakionyeshwa maeneo mbalimbali ya Benki, hapo eneo la ulinzi na usalama.
 Watoto wakionyeshwa eneo la huduma ya ATM.
 Watoto wakionyeshwa eneo la kupanga mstari wakati wa kuweka na kutoa pesa.
 Watoto wakipata viburudisho.
 Zawadi mbalimbali walizopewa watoto.
 Watoto wakiwa na zawadi zao.
 Wakati wa keki.
Mjenge mwanao mapema ili atambue umuhimu wa kuweka akiba benki, na hasa benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment