Wednesday 27 June 2018

MAWAKALA WA NMB KAGERA WAKUTANA ,WAPIGWA MSASA NA KUELEZA CHANGAMOTO ZAO.

Katika mkakati maalumu wa kuhakikisha NMB Benki inatoa huduma bora na kwa haraka kwa wateja wengi zaidi maeneo mbalimbali Nchini, Mawakala Mkoa wa Kagera wamekutana na uongozi  wa kanda ya ziwa na uongozi wa Tawi la Bukoba na kukaa pamoja na kuzungumza kwa pamoja mambo mbalimbali na changamoto zinazojitokeza katika kutoa huduma ya pesa kwa wananchi mbalimbali katika maeneo yao , Mjumuiko wa Mawakala umefanyika katika ukumbi wa St Thereza Bukoba Manispaa.(katika picha kulia mwenye Tai ni  Meneja Wakala NMB Kanda ya ziwa, wafanyakazi wa NMB Bukoba na Mawakala  kutoka maeneo tofauti.)
Tumia huduma za NMB, Ni salama na za uhakika.

No comments:

Post a Comment