Wednesday 27 June 2018

MKURUGENZI WA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI ATOA ZAWADI ZA VYAKULA KITUO CHA WAZEE KILIMA BUKOBA.

 Mkurugenzi wa viwanja vya ndege Nchini ametoa zawadi ya vyakula katika kituo cha wazee wasiojiweza lilichopo Mkoa wa Kagera Wilaya ya Bukoba, kituo hicho cha Kilima wanaishi wazee wasiojiweza wenye mahitaji mbalimbali, Akikabidhi vyakula hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa viwanja vya ndege Nchini Bi   Dorice Uhagile Meneja wa uwanja wa ndege wa Bukoba ametoa wito kwa mashirika, Taasisi na watu binafsi kusaidia vituo mbalimbali kwani serikali haiwezi peke yake, ni vizuri kuguswa na kuwa na moyo wa kusaidia kwani kila mmoja wetu ni mzee mtarajiwa.Pia Meneja alipata wasaa kabla ya Eid Liftri kupata futari ya pamoja na wafanyakazi wa Uwanja wa ndege Bukoba na wadau mbalimbali, kwa niaba ya Mkuregenzi wa viwanja vya ndege Nchini.(katika picha Meneja wa Uwanja wa ndege Bukoba Bi  Dorice  Uhagile akikabidhi zawadi kwa wazee.)
 Vyakula mbalimbali.
 Baadhi ya Wazee wanaoishi kituo cha Kilima.
 Wa pili kushoto, Meneja wa uwanja wa ndege Bukoba Bi Dorice akiwa katika kituo cha Kilima.
 Picha ya pamoja ya wazee kituo cha Kilima.
 Wada mbalimbali wakipata futari ya pamoja kipindi cha mwezi mtukufu waRamadhani.

 Picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya kufuturu.
Kwa habari za uhakika tembelea Jamcoblog.

No comments:

Post a Comment