Mjumbe
wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa
habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya
kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini
Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani
shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu
kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa
muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun.PICHA NA MICHUZI JR.
Mratibu
wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson akitoa
ufafanuzi zaidi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari
waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa
kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June
25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya
fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari
takribani 1000 hapa nchini.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta
Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii
watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma.
Mkutano ukiendelea kuhusiana na harambe hiyo.
====== ====== ====== ======
Kamati
ya Maandalizi ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee
maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health,
litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi
June 25, 2016.
Lengo
la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya
Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati ya
Maandalizi ya harambee inajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo
mbali mbali vya habari chini ya Uenyekiti wa Bw. Benjamin Thompson
Kasenyenda, inaomba ushirikiano wakaazi wa Dodoma pamoja na Wabunge.
Mtakumbuka kwamba kamati hii ilifanya tukio kama hili viwanja vya
Leaders, Jijini Dar es Salaam July 4, 2015, ambapo zaidi ya 30m/-,
zilichangishwa.
Fedha
hizo zilisaidia gharama za matibabu ya waandishi watatu waliokuwa
mahututi wakati huo, mmoja wao akiumwa kansa. Lengo la mwaka huu
limebadilika ambapo tumekusudia kuhakikisha kuwa wengi wao wanakatiwa
bima ya afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale
wanapofikwa na maradhi. Aidha, kwenye changizo hili tutakuwa na kadi
maamlum za kuomba michango ya mfuko huo, ambazo tutazigawa kwa Wabunge
kupitia ofisi ya Bunge. Tutaomba ushirikiano mzuri kutoka kwa Wabunge na
wakazi wa Mji wa Dodoma ili kufanikisha zoezi hili.
Pia
tumeandika barua kwa Spika tukimwomba awajulishe Wabunge ili wajitokeze
kwa wingi kwenye zoezi hili. Waratibu wa Harambee ile ambayo ni Kampuni
ya Media Assistant, imefanya utaratibu wa kumleta Miss Tanzania Ms
Lilian Kamazima pamoja na wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva kuja
kushiriki zoezi hilo.
Wasanii
hao ni kundi la Weusi ambalo linajumuisha John Simon Makini a.k.a Joh
Makini, Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili na George Sixtus Mdemu a.k.a G
Nako, wenye asili ya Arusha na wanafanya shughuli zao za kimuziki
Jijini Dar es Salaam pamoja na Haruna Kahena a.k.a Inspekta Haruni.
Wasanii wa Bongo Movies ni pamoja na Aunt Ezekiel, Kajala Masanja, Ray
Kigosi na Jacob Stephen a.k.a JB. Na pia kutoka Orijino Komedi tumepewa
mwakilishi Isaya Mwakilasa ambaye zaidi anajulikana kwa jina la
Wakuvanga na maarufu zaidi kama Mama Bele. Asanteni kwa Kunisikiliza
Judicate Shoo, Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee
No comments:
Post a Comment