Saturday 2 May 2015

BALOZI KAGASHEKI AISHUKURU DENMARK KWA MSAADA WA GARI LA KUZIMA MOTO MANISPAA YA BUKOBA.

 Mbunge wa Bukoba mjini balozi Khamis Sued Kagasheki ameishukuru serikali ya Denmark kupitia kwa ujumbe wa watu sita unaongozwa na Meya wa mji wa  Nykobing Mors kwa kutoa gari la zima moto katika Manispaa ya Bukoba,Mh Kagasheki akiongea kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Bukoba katika hafla fupi ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili wageni nyumbani kwake, amesema gari hili la zima moto limekuja wakati muafaka maana gari lililokuwepo lilipata ajari na bado halijafanyiwa matengenezo, amewataka waliokabidhiwa gari hilo kutambua kuwa gari hilo ni la gharama kubwa na wanao wajibu wa kutambua na kuhakikisha wanalitunza vizuri.Akiongea kwa niaba ya ujumbe aliofuatana nao Mstahiki meya wa mji wa Nykobing Mors amesema gali hili la zima moto ni  ombi maalumu lilitolewa na Mh Samwel Ntambala Rwangisa kipindi akiwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Hivyo mahusiano yake mazuri aliyoyatengeneza kati  ya Manispaa ya Bukoba na  Mji wa  Nykobing Mors kwa urafiki wa muda mrefu  ndio umezaa matunda ya kutoa msaada wa gari la zima moto.( katika picha mh Kagasheki akimtambulisha mkurugenzi wa Cosad nchini Tanzania Bw Smart Baitan.)
 Gari la zima moto liliokabidhiwa katika Manispaa ya Bukoba, ikiwa ni maombi ya Mh Samweli Rwangisa kipindi akiwa meya wa Manispaa ya Bukoba.
 Ni Bango linalothibitisha urafiki wa muda mrefu wa miji hii miwili tangu mwaka 1983.
 Wa pili kulia ni Bw Benard Matungwa, akiwa na Bw Abdul Kagasheki wakipokea wageni.
 Mzee Rutabingwa akiongoza ujumbe kutoka Denmark akipokelewa na mh Kagasheki nyumbani  kwake .
 Mh Kagasheki akimkaribisha makamu meya wa mji wa Nykobing Mors.
 Mh Kagasheki akiongea na ugeni.
 Mwenyeji wa ujumbe huu Mzee Rutabingwa akitambulisha wageni.
 Mstahiki Meya wa Mji wa Nykobing Mors akitoa neno la shukrani na kuhaidi kuendeleza mahusiano mazuri na Manispaa ya  Bukoba.
 Bw Smart Baitan.
 Mh Kagasheki akiongea na Bw Malingumu.
 Bw Jum,anne Bingwa akikaribisha wageni vinywaji.
 Mama Annamary kutoka Dernmark akimpa zawadi mh Kagasheki na moja ya kipeperushi kumuonyesha shughuli mbalimbali wanazosaidia na hasa wakina mama katika kuondokana na wimbi la umasikini.
 Bw Smart Baitan akiteta na Meya wa Nykobing Mors.
 Picha ya pamoja.
 Mzee Rutabingwa  akiongea na mtangazaji wa redio kasibante, bw Richard Kalumuna.
Jamco bukoba.blogspot inawatakia usomaji mwema wa habari  na matukio.kama una tangazo  au habari yako tupigie 0754 757157 au 0788 707027.

No comments:

Post a Comment