Monday, 27 April 2015

IDADI YA WATU WALIOFARIKI DUNIA KWENYE TETEMEKO LA ARDHI NEPAL YAZIDI KUONGEZEKA


Wanajeshi wa nchini Nepal wakiendelea kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi mjini Kathmand nchini Nepal.

Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika
katika tetemeko la ardhi mjini Kathmand nchini Nepal.

Kwa msaada wa mtandao
MAMLAKA ya nchini Nepal imesema kuwa zaidi ya watu 3300 wamesemekana kufairki dunia kutokana na Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea jumamosi katika mji wa Kathmandu nchini humo.
Waokoaji wanchi hiyo wamesema wanaendelea kuchunguza zaidi kwa kuyafikia maeneo ya mashamba mbalimbali katika mji Kathmandu, inawezekana Idadi ya watu waliopoteza maisha kuwa kubwa zaidi jinsi muda unavyozidi kwenda.

Mamia ya watu wanaoishi karibu na milima inasemekana kuwa wameachwa bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi katika nchi hiyo.

Shirika la umoja wa mataifa linalosimamia watoto (UNICEF) limesema kuwa kalibia watoto milioni moja hawana mahala pakulala, wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi pamoja na mazingira safi katika nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment