Monday 27 April 2015

WAZIRI MKUU PINDA ASISITIZA UWAZI KATIKA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI


Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kushoto kwa Waziri Mkuu na Prof. Ben Kiregyeza (kulia) ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akifungua Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.



Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi wa Kongamano la Kimataifa la masuala ya Takwimu la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa kutoka Afrika na nje ya Afrika.

Waziri Mkuu akizungumza jambo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bi. Irena Krizman leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika. Katikati ni mjumbe kutoka ya Kusini Bw. Pali Lihohla.

Waziri Mkuu akizungumza akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 32 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika.

Waziri Mkuu akizungumza akizungumza akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua kongamano la Kimataifa la Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka nchi 32 za Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika.

Waziri Mkuu akizungumza akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka nchi 32 za Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Mkutano wa siku 3 wa Takwimu jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment