Wednesday 8 April 2015

CHIPUKIZI FC YA ISHOZI YATWAA UBINGWA WA MSAFIRI MATELEPHONE CUP,JULIUS RUGEMALIRA MGENI RASMI.

 Wa kwanza  kulia Bw Msafiri Matelephone wa Ishozi muandaaji wa mashindano akiwa na mgeni rasmi Bw Julius Rugemalira ,Mashindano haya yalijumuisha timu mbalimbali za mpira wa miguu,timu ya wazee mpira wa miguu, mashindano ya kukimbia mita mia moja kwa wazee, wanawake na vijana,zawadi za  zaidi ya milioni moja na nusu zilitolewa na mgeni rasmi kwa washindi mbalimbali.Mgeni rasmi Bw Julius Rugemalira alitoa zawadi  za washindi katika michezo yote kiasi cha zaidi ya milioni moja na nusu, katika hotuba yake amesisitiza upendo na ushirikiano na watu kuwa na tabia ya kushiriki michezo kwa watu kufurahi na kujenga afya.
 Mgeni rasmi akisalimiana na mmoja wa washindi katika mita mia moja Bw Faustine Kagonzi akikabidhiwa  zawadi.
 Bi Jamida swalehe mshindi wa mbio mita mia moja kwa upande wa wanawake.
 Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na timu ya wachezaji wa timu yawazee,
 Ilikuwa burudani kweli , mzee akikata mbuga akiwa peku,.
 Hapana chezea mzee Yasini akimzibiti adui na ndio alikuwa nyota wa mchezo aliifungia timu yake bao moja.
 Kikosi kamili cha  Ishunju Fc washindi wa pili.
 Ishunju Fc na mgeni rasmi na viongozi mbalimbali katika picha.
 Chipukizi Fc mabingwa wa  kombe la  Msafiri Matelephone cup Ishozi 2015, walijinyakulia zawadi ya 600,000 cash kutoka kwa Bw Julias Rugemalira.
 Bw Edison Mtalemwa akisisitiza kitu.
 Wapenzi wa soka wakifuatilia soka.
 Mashabiki wa chipukizi Fc wakishangilia goli.
Endelea kufuatilia jamcobukoba.blogspot.com

No comments:

Post a Comment