Sunday 9 November 2014

JK AFANYIWA UPASUAJI MDOGO AENDELEA VYEMA NA MATIBABU NCHINI MAREKANI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, jana Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume.



Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. Tutaendelea kuwashirikisha taarifa ya maendeleo yake
mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment