TIMU ya Kashai Fc maarufu kama Abanyaruganda imetupwa nje ya Mashindano ya Ligi ya Kagasheki leo kwenye Hatua ya Robo fainali baada ya kutoshana nguvu ya bao 1-1 na timu ya Miembeni. Kipindi cha kwanza kilimalizika ya bila kufungana. Timu ya Kashai ndio ilianza kupata bao katika kipindi cha pili kupitia mchezaji wake Shamte Odilo na wao Miembeni kusawazisha bao kupitia kwa Rashid Mandawa katika kipindi hicho hicho cha pili na mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 na hatimaye Mtanange kwenda kwenye Mikwaju ya penati ambayo timu ya Miembeni imeibuka kidedea kwa penati 5-4. Ushindi huu wa Timu ya Miembeni unawakutanisha na Mabingwa watetezi Bilele Fc walioshinda jana bao 1-0 timu ya Kahororo na sasa watakutana katika Nusu Fainali wiki Ijayo kati ya Bilele Fc na Miembeni walioshinda leo.
Ilikuwa ni Ngoma na Nyimbo kwa Mashabiki hawa wa Kashai maarufu Abanyaruganda
Mizuka ya Mashabiki wa Kashai Fc wakiipamba timu yao leo kwenye mchezo wake wa Robo Fainali dhidi ya timu ya Miembeni Fc
Viongozi wakiwa Jukwaa Kuu wakitazama Mtanange kati ya Kashai Fc vs Miembeni Fc, wa pili kutoka kulia ni Bw. Ernest Nyambo.
Mashabiki Jukwaa kuu wakitazama Mtanange!
Mashabiki wa Kashai wakiishangilia timu yao leo hii ambayo imetupwa nje kwa mikwaju ya penati baada ya kuchezea sare ya 1-1 za dakika 90.
Kisa Mwamuzi Mshika kibendera alinyanyua kuashiria kuotea huku wachezaji wa Miembeni wakipingana nae!!
kabla ya Timu ya Mimbeni hawajapata bao walikwaruzana na Mwamuzi wa pembeni mshika kibendera..
Wachezaji wa Miembeni wakishangilia bao lao la kusawazisha lililotiwa kimiani na Rashid Mandawa
Wachezaji wa Miembeni wakicheza Muziki baada ya kusawazisha bao katika kipindi cha pili kwa kufanya 1-1 ndani ya dakika 90.
Ilikuwa ni staili ya aina yake kushangilia
Nyomi ya Mashabiki Uwanjani Kaitaba wakitazama Mechi ya leo hii kati ya Kashai Fc na Miembeni
Mashabiki wa Timu ya Kashai wakitokelezea!! 

Mashabiki wakitazama Kipute cha leo hii
Katika Michuano hii ya Ligi ya Kagasheki 2014 Kata ya Kashai ndio huwa na Mashabiki wengi
No comments:
Post a Comment