Shekhe wa Mkoa wa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta amekemea viongozi wa kidini na siasa kuwa waangalifu na kauli zao kwa wananchi zinazoweza kuhatarisha amani nchini.Akiongea na waislamu walioswali katika msikiti wa Jamia Manispaa ya Bukoba leo katika kuazimisha sikukuu ya Edd el-ftr,Shekhe Haruna amesema si busara na haitakiwi kabisa viongozi wa dini au siasa kuchochea na kuhatarisha amani ya nchi hii kwa masilahi yao binafsi.Pia katika salamu zake za Idd amewataka wabunge wa bunge la katiba waliosusia kikao watambue kuwa wapo pale kwa ajiri ya wananchi hivyo kususia Bunge si Busara kwani wenye kauli ya mwisho ni Wananchi wa Tanzania na si wao, hivyo ni vema wakarejea Bungeni kuendelea na vikao.
Waumini wakisikiliza mawaidha ya Idd
Hali ya usalama iliimarishwa ili waumini waweze kuswali kwa amani na utulivu
Mc Baraka ndani ya kanzu lake akitinga msikitini
Ni furaha tu za Idd
Shekhe Kakwekwe akieleza jambo
Mapacha hao
Maurana akiwa na wanae
mtaani baada ya swala
Seneti nako tukapita, hali ilikuwa hivi.
Familia mbalimbali baada ya kuswali
Mama na wanae akataka atokelezee kwenye blog.
Pilika lango kuu la soko.
Akataka apate picha,nasi bila hiyana tukapiga.
Ni benz ya zamani ya Marehemu Rostamal Radha likiwa na mjuu wake mtaani wakitokea msikitini
Ni kuwahi sokoni
Ni pilika baada ya swala ya Idd
Kifamilia zaidi
Mr Mohamed Remdin akiwa na mke wake Rehana wakifurahi na camera yetu mitaa ya Miembeni baada ya swala ya Idd
No comments:
Post a Comment