Bw Amos Rweyemamu ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika mahafari ya darasa la saba shule ya msingi Igoma akiongea na wazazi na wageni waalikwa,amewataka wazazi kushirikiana na serikali kusaidia kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi waweze kusoma vizuri,bw amos baada ya kutembelea majengo ya shule na kujionea hali mbaya ya baadhi ya madarasa yakiwa yameharibika sakafu na watoto kusomea katika vumbi ,ameahadi kuvifanyia ukarabati vyumba hivyo haraka iwezekanavyo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri,pia ameahidi kununua ngoma za bendi ambazo zimeharibika.bw Amos anaeishi nchini spain amesema wanao umoja wao huko spain wenye watu kama 200 unajinyima kidogo wanachokpata na kusaidia watoto wenye mahitaji,yatima na walioadhilika na virusi vya ukimwi,amewasihi watanzania kuwa na moyo wa kizalendo wa kusaidia wahitaji.
hili ni mojawapo ya darasa ambalo limeharibika sakafu,ambalo wanafunzi wanalitumia na ni hatari kwa afya zao,bw amos amejitolea kukarabati,lakini jitokezeni na wengine kusaidia mahitaji ni makubwa sana shule imejengwa miaka zaidi ya 50 iliyopita.
mgeni rasmi akionyeshwa hali halisi ya madarasa
wanafunzi wakiingia katika ukumbi wa mahafari ya darasa lasaba
wazazi katika mapozz tofauti
mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni
waalimu katika pozzz
ni wahitimu 47 wakifurahia
chezeeaa darasa la tatu weweee
watoto mahiri katika burudani ya taarabu wakiwaaga wenzao
risara ya wahitimu ikakabidhiwa kwa mgeni rasm ili ijibiwe
mgeni rasmi akapewa zawadi ya jogoo alienona
wahitimu katika miondoko ya kwaito...
mwalimu mkuu wa shule ya igoma akiwasihi wahitimu kuwa watulivu na kuendelea na masomo ya pre form one wakisubiri matokeo yao
burudani kama kawaida
mmoja wapo ya wazazi wakiwa na mtoto wao aliehitimu darasa la saba
No comments:
Post a Comment