Ilikuwa ni siku ya pekee sana katika familia ya
Omurangila Justuce Rugaibula ya kukutanisha watoto yatima wa kituo cha
Nusuru kilichopo Kashai Manispaa ya Bukoba, ndugu ,jamaa na marafiki na
kufuturu kwa pamoja,na baada ya hapo ilisomwa dua ya kumshukuru mwenyezi
mungu kwa mema na makuu anayoitendea familia,Hafla hii fupi ya kufuturu
ilifanyika nyumbani kwa Omurangila Justuce Rugaibula Ibura katika kata
ya Ijuganyondo.Kwa niaba ya Bw Justuce Rugaibura ambae akuwepo yupo
safarini nje ya nchi, mama Mzazi Ma Graice alitoa neno la shukrani kwa
wageni wote waliofika katika hafla ya kufuturu na watoto yatima, na Ma
Graice alitoa wito na kuwaomba wadau mbalimbali kusaidia watoto yatima
kwani ni wajibu wa kila mmoja kutambua na kuona kuwa anayobudi ya
kusaidia .(katika picha watoto yatima , ndugu na marafiki wakiomba dua.)
Makazi ya Omurangila Justuce Rugaibula ,.
Shekhe wa wilaya Bukoba Mjini ,Shekhe kakweke akipata futari na wageni wengine.
Kushoto Bw Emily Baruti na Bw Arodi Baruti wakipata Futari.
Wadau mbalimbali waliobahatika kufika wakipata futari.
Rais wa Kanda ya ziwa akihakikisha kila mtoto anapata chakula na kinywaji.
ILIHAM CAFE,Wataalamu wa kupika vyakula mbalimbali katika shughuli mbalimbali ,ndio waliandaa futari.
Bw Rahim Kabyemela akiwajibika ipasavyo kuhakikisha watoto wanapata huduma.
Rais wa kanda ya ziwa alilazimika kuwa karibu na huyu mama washirikiane kutoa huduma.
Kulia Bw Afidhu Karugila,mtu muhim sana aliehakikisha shughuli zinakwenda vizuri. akiwa na Bw Novatus Nkwama mwenyekiti mstaafu wa ccm Bukoba vijijini.
Kulia Ma Graice akionekana na furaha.
Rais wa kanda ya ziwa baada ya shughuli nzito.
Kijana Rama ,mdau mkubwa aliehakikisha shughuli inafanikiwa.
MA OGARNAISER.
KWA HABARI ZA KIJAMI, BURUDANI NK TEMBELEA BLOG YETU. AU PIGA SIMU 0788707027 AU 0754757157
No comments:
Post a Comment