Sunday, 8 October 2017

NMB WAJIBU KILIO CHA WATEJA WAO BUKOBA,WAFUNGUA TAWI JIPYA LA KAITABA.

 Baada ya Mkoa wa Kagera shughuli za maendeleo kuonekana kukua na hivyo mahitaji ya huduma za kibenki kuhitajika, Benki ya NMB  imeliona hilo na kulipa umuhimu mkubwa na kusikiliza kilio cha wanachi na wateja kwa kuongeza tawi  lingine katika Manispaa ya Bukoba  tawi la Kaitaba.Katika hafla ya ufunguzi ,mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera  Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu, ameushukuru uongozi wa NMB kwa kujari wateja wake na kuwataka wananchi wa Kagera kuchangamkia fursa hii na hususani wakazi wa Bukoba mjini na maeneo jirani.Nae Mkurugenzi wa NMB  Bi  Ineke Bussemaker  amesema nia ya NMB ni kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi na kusogea karibu na wanachi kwa kufungua matawi mengi zaidi na kutumia huduma mbalimba kupitia kwa mawakala, m pesa kwa kutumia simu za mikononi ili kumraisishia mteja kupata huduma kwa haraka.katika picha ( kulia Mkurugenzi NMB Bi Ineke Bussemaker, Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Salum Mustaf Kijuu akikata utepe, Mjumbe wa bodi  Bw Protase Tehingisa na Kaimu Afisa wa wateja wadogo na wa kati Abdulmajid Nsekela.)Fuatilia tukio zima picha 131.
 Muonekano wa jengo la tawi la Kaitaba.
 Mc Jerry alieongoza shughuli nzima.
 Muonekano eneo la ndani.
 Eneo la ndani.
 Wafanyakazi wa NMB Bukoba katika pozz.
 Meneja Mahusiano wa NMB katika ubora wake.
 Mkurugenzi NMB (kushoto) akiwasili  eneo la tukio akipokelewa na meneja tawi la Bukoba.
 Wafanyakazi wa NMB.
 Mkurugenzi wa NMB akivishwa kitenge, na mmoja wa wafanyakazi wa NMB BUKOBA.
 Picha ya pamoja wafanyakazi wakiwa na Mkurugenzi wa NMB.
 Mkurugenzi akisalimiana na wateja.
 Kushoto Bw Mushobozi , meneja mstaafu wa tawi la Bukoba, Meneja wa tawi la Bukoba kwa sasa na Mkurugenzi NMB wakisalimiana.
 Mgeni rasmi akiwasili eneo la tukio.
























Kwa mahitaji ya video, picha na mnato, kurushwa mtandaoni jamcobukoba.blogspot.com tupo kwa ajili yako, tupigie simu  0788-707027, 0754-757157 au 0622-757157.

No comments:

Post a Comment