Monday, 21 August 2017

KITENDAGURO WAWA MABINGWA BONANZA LA JAMBO BUKOBA 2017,50,000,000 ZATOLEWA, KUNA MAISHA BAADA YA TETEMEKO.

 Ilikuwa ni shangwe, furaha isiyokifani kwa wanafunzi,walimu na wananchi wa kata ya Kitendaguro Manispaa ya Bukoba walipoibuka kidedea katika bonanza la michezo lililoandaliwa na shirika la kukuza vipaji vya michezo watoto wa shule za msingi Mkoa wa Kagera  Jambo Bukoba,Bonanza hilo lililoshirikisha shule kumi kutoka Manispaa ya Bukoba na Bukoba vijijini kwa wale waliothirika na Tetemeko la ardhi lilotokea mkoani Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu na kupelea vifo 17,Bonanza hilo lililobeba kauli mbiu ya (KUNA MAISHA BAADA YA TETEMEKO)yaliongozwa na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh Deodatus  Kinawilo,Mkurugenzi wa Jambo Bukoba Bw Clemens Mulokozi mbali ya kutoa zawadi mbalimbali zikiwemo jezi, mipira na vikombe kwa mshindi wa kwanza mpaka watatu alitoa kiasi  cha shilingi milioni tano kwa kila shule ili  zisaidie kuboresha miundombinu iliyoathirika wakati wa Tetemeko,hivyo ametoa kiasi cha shilingi milioni hamsini kwa shule kumi. Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Gymkana Bukoba Manispaa liliuzuriwa na viongozi mbalimba wa serikali na wananchi kwa ujumla.(katika picha mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi kitendaguro Joel Byolwango akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi.)
t

( Kulia) Mkuu wa wilaya Mh Deodatus Kinawilo akiwa na mkurugenzi wa Jambo Bukoba Bw Clemens Mulokozi.
 Bw Gonza, Meneja wa Jambo Bukoba.
 Wafanyakazi wa Jambo Bukoba.
jamcobukoba.blogspot.com inakushukuru Bw Clemens Mulokozi kwa kukuza michezo mashuleni , na kusaidia shule zilizoathirika na TETEMEKO.

1 comment: