Monday, 13 February 2017

WAKAZI WA MANISPAA YA BUKOBA WAAGA MWILI WA OMWAMI TA EMMANUEL R.G. MUTABUZI,KUZIKWA JUMATATU 13-2-2017 KASHABA KYAKA.

 Wakazi wa Manispaa ya Bukoba wamefurika kwa wingi kushiriki ibada takatifu ya kumuaga Omwami Emmanuel Mutabuzi aliefariki 9-2-2017 na atazikwa 13-2-2017 kijijini kwao Kashaba Kyaka.Waumini mbalimbali kutoka maeneo tofauti waliudhuria Ibada iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kashai Bukoba iliyoongozwa na baba paroko Padre Faustine Kamuabwa, Baba paroko alitumia maubiri yake kuwasihi waumini kumcha mungu na kuwa waadirifu, wakweli, waungwana na kuishi vizuri katika jamii,Mara baada ya ibada msafara uliondoka kuelekea kijijini Kashaba Kyaka kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatatu 13-2-2017.
 Ni hospital ya Mugana  chumba cha kuifadhi maiti,
 Ni wakati mgumu kwa watoto wa marehemu na wanandugu.
 Kushoto ni mtoto wa marehemu Wilbroad Mutabuzi akiwa na kaka yake.
 Kushoto mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna akitoa maelekezo.
 Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Wilfred Rwakatare, rafiki wa karibu wa familia ambae aliongozana na wanandugu akitokea bungeni Dodoma kuja msibani.
 Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake Kashai, ukitokea Mugana hospitali ulikokuwa umeifadhiwa.
 Bw Medard Kaijage mwenyekiti wa kamati ya mazishi.
  Kulia Mh Mbunge Saverina Mwijage akiwa na Bi Domina Arodi Baruti.
 Wanafamilia.
 Bw Bushira akiwa kazini.
 Idada ikianza.
 Mh Mbunge Saverina Mwijage.
 Familia wakiaga mwili wa marehemu.
 Mwili ukipelekwa kijijini kwake Kashaba Kyaka.
 Mwili wa marehemu umewasili nyumbani kwake Kashaba Kyaka na mazisho ni tarehe 13-2-2017 siku ya Jumatatu.
 Green gard wa ccm wakiwa wamebeba jeneza la marehemu.
 Ndugu na jamaa wakilia kwa machungu, mara tu mwili ulipowasilli nyumbani kwake Kashaba Kyaka.
 Mjane wa marehemu akilia kwa machungu.
 Kushoto ni mwenyekiti wa ccm mkoa kagera Mama Constancia Buhiye akiwa na mme wake.
Endelea kufuatilia jinsi ya mazishi yatakavyofanyika, jamcobukoba.blogspot.com  inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote.

No comments:

Post a Comment