Sunday 11 September 2016

WAZIRI MKUU AWASILI BUKOBA,ASHIRIKI SALA YA KUWAAGA MAREHEMU WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA.

 Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amewasili  leo mchana katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa ajili ya kuwapa pole waanga wote na waliopoteza jamaa zao katika tetemeko kubwa la ardhi lilitokea katika mkoa wa Kagera 10-9-2016 majira ya saa 9.30 jioni na kusababisha maafa makubwa.Katika tetemeko hilo ambaalo kwa kiasi kikubwa limeathili katika manispaa ya Bukoba watu 16 mpaka sasa wamepoteza maisha,majerui zaidi ya 150 wapo katika hospitali ya mkoa, na zaidi ya mia moja wameruhusiwa kurejea nyumbani,Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu amesemazaidi ya nyumba 800 za wananchi zimebomoka kabisa, nyumba zaidi ya 1000 zimeathirika kwa kupata nyufa naa uharibifu mwingine,hivyo kinachoendelea kufanyika kwa sasa ni kupata takwimu zilizosahihi zaidi ili iziwasilishe serikalini, kwa hatua ya awali serikali imenunua majeneza kwa marehemu , sanda na kutoa usafiri kusafirisha marehemu katika maeneo watapozikwa,Waziri mkuu Kassim Majaliwa alianza kwa kuwapa pole wananchi kwa tukio la aina yake kutokea nchini Tanzania kwa mara ya kwanza na kuacha maafa makubwa,amesema timu ya kitengo cha maafa itawasili leo mkoani Kagera ili ishirikiane na viongozi waweze kupata takwimu sahihi ili serikali iweze  kusaidia.
 Viongozi wakiwa uwanja wa ndege Bukoba.
 Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wilfred Rwakatare akimkaribisha waziri mkuu.
 Mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna akimkaribisha waziri mkuu uwanja wa ndege Bukoba.
 Waziri mkuu akiongea na viongozi, baada ya kupata taarifa kutokaw kwa mkuu wa mkoa.
 Waziri mkuu akiwasili hospitali ya mkoa wa kagera akipokelewa na viongozi.
 Waziri mkuu Kasimu Majaliwa akiwapa pole wahanga ktk hospitali ya mkoa wa kagera.
 Mama na mtoto , wahanga.
 Bi Hidaya Kashinde mhanga aliumia sana.
 Wodi wa wahanga wanaume.
 Baadhi ya majeneza ya miili ya marehemu.
 Waziri mkuu akiwasili katika uwanja wa mpira wa miguu Kaitaba.
 Red cross wamefanya kazi kubwa.
 Majeneza ya miili ya marehemu.
 Mwenyekiti wa ccm Mkoa Wa Kagera Costansia Buhiye akitoa pole kwa wananchi wote wa mkoa wa Kagera kwa niaba ya chama cha mapinduzi.
 Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Wilfred Rwakatare akitoa pole kwa wananchi, na kuiomba serikali kusaidia kupumguza vifaa vya ujenzi kwa kipindi maalumu kwa wale wote waliathirika na tetemeko.
 Mbunge viti maalumu Saverina Mwijage akiongea na wanachi kutoa pole.
 Mstahiki Meya Manispaa ya Bukoba akiongea na wananchi.
 Waziri mkuu akiongea na maelfu ya wananchi wa mkoa wa kagera katika uwanja wa kaitaba Bukoba Manispaa.
 Waandishi wa habari vyombo mbalimbali wachukua matukio.
Waziri mkuu akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.

No comments:

Post a Comment