Saturday 17 September 2016

MWANAMITINDO NA MSANII MAARUFU JOKATE(KIDOTI) NA GSM FOUNDATION WATOA MSAADA MAGODORO 400.

 Mwanamitindo na msanii maarufu nchini Tanzania Jokate Mwengelo(Kidoti)amefika leo 17-9-2016 katika Manispaa ya Bukoba akiiwakilisha kampuni ya GSM Faundation na kutoa msaada wa Container zima la magodoro 400 kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi lillilotokea Mkoani Kagera tarehe 10-9-2016 na kusababisha vifo,majerui na nyumba kubomoka. Mwana kusema mitindo Jokate akiongea kabla ya kukabidhi msaada alimueleza mkuu wa mkoa wa Kagera  kuwa Baada ya tukio hilo kutokea aliguswa na alikwenda GSM Faundation kuwaomba na anashukuru awakusita maana wamekuwa wakifanya shughuli za kijamii kila mara,aliendele akusema ameona afike mwenyewe aweze kuona namna wahanga walivyoathirika .(katika picha Jokate akikabidhi magodoro 400 kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu.)
 Katikati ni mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Yahaya Kateme mwakilishi wa GSM Kagera, akishuhudia Katibu wa uvccm Mkoa Ddas Zihimbile akikabidhi fulana za GSM kwa Mwanamitindo Jokate.
 Mtangazaji wa Clouds Tv  Siza akifanya interview na Jokate.
 Jokate akifanya Interview na waandishi wa vyombo mbalimbali.
 Jokate alitembelea ghala linalohifadhi vitu mbalimbali vinavyotolewa  na watu mbalimbali kwa ajili ya wahanga.
Jamcobukoba.blogspot.com inatoa wito kwa wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia, maana mahitaji ni makubwa sana.

No comments:

Post a Comment