Thursday, 18 August 2016
RUNGU LA WAZIRI LUKUVI LATUA KWA MWEKEZAJI GEORGE ROGERS KUFUTA UMILIKI WA ARDHI
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi akipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salumu Mstapha Kijuu akimkaribisha waziri alipowasili katika ofisi ya mkuu wa Kagera.
Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amebatilisha umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 200 iliyoko katika maeneo ya Kibuye, Bugolola na Nyanga ambayo mwekezaji George Rogers Mtanzania mwenye uraia wa Uingereza ambae ni mmiliki wa kampuni ya Rockshiel Quality Food Processors Limited alitaka kuitaumia kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama, Waziri Lukuvi ambae yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kutatua kero mbalimbali za migogoro ya ardhi mkoani Kagera,ametoa uamuzi huo wakati alipokutana na wananchi wa mkoa wa Kagera kwenye viwanja vya Halmashauri ya wilaya ya Bukoba kwa lengo la kusikiliza kero zao zinazohusiana na masuala ya ardhi, amesema mwekezaji huyo hana sifa za kumiliki ardhi hiyo kwa kuwa sio raia
wa tanzania hivyo alipaswa kuomba ardhi kupitia
kituo cha uwekezaji nchini (TIC) jambo ambalo mwekezaji huyo alilipinga, Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyanga,wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa mwekezaji huyo alikuwa akiwatishia maisha wale wote waliokuwa wakihoji uhalali wa kupata hiyo ardhi kwa kuwa sehemu ya ardhi aliyokuwa akimiliki alikuwa ameipora kwa nguvu,naye mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salumu Mustapha Kijuu amemueleza waziri kuwa asilimia 80 ya migogoro inayotishia usalama na amani mkoani Kagera inahusiana na masuala ya ardhi.(katika picha ni mwekezaji George Rogers)
Waziri akiwasili eneo la mkutano katika viwanja vya Halmashauri ya Bukoba kuzungumza na wananchi.
Afisa ardh Manispaa ya Bukoba, Bw Mwamsojo akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo .
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment