Monday, 1 August 2016

MUFTI WA TANZANIA AWATAKA WAUMINI WA KIISLAMU WAJITAMBUE KWENYE ELIMU NA UCHUMI,WAZIRI MWIGAGE ASEMA MILANGO IKO WAZI.

 Mufti wa Tanzania Abubakari Zuberi amewataka waumini wa dini ya kiislamu kujitambua kwenye swala la elimu na uchumi,Mufti amesema kwa muda mrefu sana waumini wa kiislamu wamekuwa nyuma katika elimu na swala zima la uchumi,Mufti amesema wakati umefika wa kutambua kuwa dunia inabadilika kwa kasi sana, hivyo ili uweze kwendana na kasi ni lazima elimu na uchumi viende kwa pamoja, Mufti aliyasema haya wakati wa shirikisho la wasoma maulid Tanzania lilofanyika  Bukoba kwenye chuo cha kuifadhi kuruani Busimbe katika kata ya Kitendaguro Bukoba,Pia Waziri wa viwanda  na Biashara Charles Mwijage alipata fursa ya kuwaeleza wanashirikisho na waalikwa wote kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati bila kurudinyuma kuhakikisha Tanzania ya viwanda vya kati na vidogo inafanikiwa, hivyo ametoa wito na kuwahimiza serikali iko kwa ajili yao bila kujari dini, kabila wala itikadi za vyama vya kisiasa, kazi aliyonayo ni kuhakikisha kile anachotarajia mkuu wa nchi kinatimia na wananchi wa tanzania kuondokana na umasikini.

 Kulia ni shekhe wa mkoa kagera Haruna kichwabuta, Waziri wa viwanda na biashara charles Mwijage, Mwenyekiti wa Bakwata mkoa wa kagera Alhaj Abubakari Kagasheki,Mwenyekiti wa shirikisho la wasoma maulid Tanzania Adlarah Fuu Jafari na alhaj Amir Amza mkurugenzi wa kiwanda cha Amirs Amza,
 Mufti wa Tanzania Aubakari Zuber (kushoto) akiwa na mwenyekiti wa shirikisho Tanzani wasoma maulid Abdalar Fuu Jafar.

No comments:

Post a Comment