Thursday 11 February 2016

MWENYEKITI WA BUKOBA VETERAN SEIF MKUDE AWAASA WANAWAKE KUPENDA MICHEZO.

Mwenyekiti wa Bukoba veteran Bw Seif Mkude amewataka wanawake kupenda michezo mbalimbali kwa ajili ya afya zao na kuburudika,Bw Mkude aliyasema hayo hivi karibuni kwewnye sherehe ya kuaga na kukaribisha mwaka mpya iliyoandaliwa na wanawake mbalimbali wapenda michezo wa Manispaa ya Bukoba, Mgeni rasmi Bw Mkude aliwaomba wanawake wajiunge na Bukoba veteran ili waweze kujifunza na kujua mengi kuhusiana na michezo, sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kiroyera beach.
Wachezaji wa timu ya mpira wa pete katika ubora wao.
Kulia ni Bi Zaitun akiwa na BI Rebecca wapenda michezo.
Mwenyekiti wa sherehe Bi Zaitun akieleza umuhimu wa kukutana katika siku  hii ya sherehe.
Kocha Nora, ni mwalimu wa muda mrefu sana katika mpira wa pete mkoa wa Kagera.
Watu wakaburudika.
Mchezaji maarufu katika mpira wa wavu.
Ikakatwa keki.
Mgeni rasmi akimlisha keki Katibu wa chaneta Mwl Revina.
Shampeen ikafunguliwa.
Cheereess
Kushoto ni mchezaji mkongwe

No comments:

Post a Comment