Thursday 24 September 2015

WAZIRI KOMBANI AFARIKI:


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani amefariki leo jioni katika hospitali ya Apollo nchini India alikokwenda kutibiwa, vyanzo kutoka serikalini vyathibitisha.
Kombani alikuwa anagombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mwanasiasa huyo, Celina Kombani amezaliwa Juni 19, 1959 na ameliongoza jimbo la Ulanga Mashariki tangu 2005.
Kabla ya kurudishwa katika Ofisi ya Rais, marehemu Celine Kombani alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba.

No comments:

Post a Comment