Thursday 24 September 2015

UCHOMAJI MAKANISA, SERIKALI KAGERA YAINGILIA KATI.



. Viongozi wa makanisa hayo kuwa washirika namba moja,
. Umoja wa makanisa ya Kipentekoste wahitaji mwongozo.
Wakati serikali mkoani Kagera, ikikagua makanisa hayo na wahakikishia wachungaji na waamini wa makanisa yaliyochomwa moto katika manispaa ya Bukoba , wachungaji waomba mwongozo wa aina gani ya makanisa wajenge ili yaheshimiwe.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea Makanisa yaliyochomwa moto, mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani  Kagera JOHN MONGELA, amesema kuwa tayari polisi imeanza kuwatafuta waliohusika na matukio hayo.
Bwana MONGELA ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kagera, amesema kuwa kwa nchi kama Tanzania,  vitendo hivyo vinatakiwa kukemewa na kuwaomba wachungaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki,  ambacho serikali inaendelea kulishughulikia.
Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste –PCCT-,  mchungaji CRODWARD EDWARD ameishukuru serikali ya mkoa kwa jinsi inavyoendelea kulishughulikia.
Mchungaji EDWARD amesema kuwa kutokana na makanisa hayo kuwa yanachomwa moto, wameaanza kupoteza imani na serikali lakini kutembelewa na mkuu wa mkoa sasa wana imani suala hilo litashughulikiwa.

No comments:

Post a Comment