Monday 3 August 2015

MKUU WA MKOA KAGERA AWATAKA WAJASIRIAMALI KUWA NA NIDHAMU NA PESA ZA MIKOPO,ESAURP NA FSDT WAENDESHA MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI BUKOBA.

 Zaidi ya wajasiriamali 150 wa Bukoba wanaojishughulisha na utalii na shughuli nyingine za biashara wameanza mafunzo ya ujasiriamali kwa ajiri ya kujenga uwezo wa kuhuisha biashara zao.Mradi  URPhuu unaofadhiliwa na taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini (FSDT) na  kutekelezwa na program ya utafiti ya vyuo vikuu vya nchi za mashariki na kusini mwa Afrika (ESAURP) ni mwendelezo wamradi  huo uliotekelezwa mwaka 2013 na ESAURP ambapo safari hii unalenga kufikia mikoa kumi ya Arusha, Kilimanjaro,Mbeya,Iringa,Kagera, Mtwala, Kigoma, Singida, Morogoro na Dodoma.
 Washiriki wa mafunzo..
 Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa ESAURP Prof  Ted Maliyamkono akiwa na mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongella.
 Msimamizi wa ESAURP Bukoba Bw Mutakyahwa Ruta.
 Meneja wa ESAURP Bi Flolentina .C. akieleza namna wanavyofanya kazi katika kujenga uwezo wajasiriamali.
 Prof Ted Maliyamkono amesema kazi kubwa wanayofanya kama ESAURP katika Mradi   unalenga kusaidia biashara  ndogo ndogo na za kati zinazoendeshwa katika mfumo usio rasmi kupata uwezo na maarifa ya kusaidia kukua na kuwa sekta rasimi,kupata huduma za kifedha,pia kufahamu benki washiriki ili kutengeneza mabadiliko ya tamaduni za kibenki namna ya kusaidia miradi ya sekta isiyo rasimi katika miradi inayotafuta huduma za kibenki na hasa mikopo.Bw Christian Mpalanzi  Mtaalamu mshauri wa huduma za Fedha kwa wajasiriamali(FSDT) taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella akifungua mafunzo ya ujasiriamali,amewsaataka washiriki kuzingatia mafunzo na kuheshimu na kuwa na nidhamu na pesa za mikopo.
 Wajasiriamali 150 walishiriki mafunzo katika ukumbi wa St Francis Bukoba.
 Mmoja wa washiriki.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na waandaaji wa mafunzo.
 Mgeni rasmi akiwa na wajasiriamali.
Endelea kufuatilia jamcobukoba.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment