Ni mh Bernadeta Mushashu katika picha akitumbukiza kura kwenye sanduku,Kura hiyo ilikuwa inakamilisha idadi ya kura 432 alizopata kwenye kinyanganyiro cha nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Kagera UWT CCM,Katika kipindi kilichopita Mh Mushashu alikuwa nafasi ya pili na alibahatika kuwa mbunge viti maalum, Kwa kipindi kilichopita MH Elizabert Batenga alichukua nafasi ya kwanza na sasa amekuwa wa tatu kwa kupata kura 255,na nafasi ya pili kuchukuliwa na Bi Oliva Semugukuu mwenye umri wa miaka 30 na ndio kagombea kwa mara ya kwanza,Mh Batenga alipopewa nafasi ya kushukuru wajumbe aliwashukuru kwa kumchagua kwa kipindi cha miaka 25 mfululizo na kuwaaga rasmi wajumbe,Nafasi ya nne ilichukuliwa na Bi Janath Musa ambae ni katibu wa ccm Mkoa wa Tabora aliepata kura 133.
Muonekano wa wajumbe ukumbi wa jengo la ccm Mkoa wa Kagera ambalo halijamalizwa kujengwa kwa muda mrefu sasa.
Kulia Bi Janath Musa.
Mwenyekiti wa ccm Mkoa Kagera Mama Buhiye akifungua Mkutano.
Katibu wa ccm Mkoa Bw Amie akitoa maelekezo.
Mkuu wa Mkoa Kagera akiingia ukumbini.
Mkuu wa Mkoa Kagera John Mongella,ambae alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi .
Binti mdogo Godeleva Kaijage kupitia vyuo vikuu aliibuka kidedea kwa kupata kura 487.
Magoti yakapigwa wakati wa kuomba kura.
Mama Elizabert Batega baada kura kutotosha akishukuru na kuaga rasmi wajumbe.
Wapambe wa mama Mushashu kwa raha zao.
Mme wa Mama MUSHASHU AKIMPONGEZA MKE WAKE KWA USHINDI.
Mke wangu wewe ni zaidi ya jembe wewe ni burudoza, leo umevunja rekodi, oba mukazi we manzi.
Mtoto akiwa na furaha, mama kashinda,Hongera Kemi.
CCM NI ILE ILE, WATU WAKAKATA MAUNO.
Vyomba vya habari vikamuhoji mshindi.
Akaeleza kilicho moyoni, kikubwa ni furaha ya ushindi na kutafuta kura za ccm ili safari yake ikamilike.
Oliva Semugukuru wa tatu kulia na mmewe wa kwanza kushoto wakiwa na wapambe wao wakifurahia ushindi wa pili.
No comments:
Post a Comment