Monday 9 March 2015

KULIKONI KATA KITENDAGURO NA KIBETA, HAWA WAUAJI IMESHINDIKANA KUPATIKANA? ,WANANCHI WAONYESHA WOGA NA WASIWASI MKUBWA MAJUMBANI MWAO.



Miili ya vijana hao ikiwa kwenye gari la msamalia mwema tayari kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.
 
Vijana wawili wamekutwa wamefariki katika maeneo tofauti kwenye kata ya Kibeta na Kitendaguro manispaa ya Bukoba.
Wakizungumza katika eneo la tukio wenyeviti wa mitaa ya Kagemu pamoja na Kanazi,............
wamesema kuwa wananchi wameshuhudia tukio hilo leo alfajiri.
Mmoja wa wenyeviti hao  Bwana Oscar Morika amesema kuwa marehemu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Egid amekatwa katwa mapanga katika maeneo mbalimbali ya mwili wake hasa kichwani na sehemu nyingine.
Aidha wenyeviti hao wamesema kuwa kutokana na mauaji hayo wameamua kukaa na kuweka ulinzi wa pamoja katika kukomesha mauaji hayo.
Kwa upande wake mkuu wa upelelezi mkoa wa kagera bwana GIRESO MROTO amesema kuwa kutokana na mfululizo wa mauaji hayo wananchi inabidi kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwabaini wahalifu, huku akiaidi polisi kutoa taarifa kamili.
Bwana Mroto amesema kuwa katika mauaji hayo, inabidi kuwekea mkakati wa pamoja ili waweze kukomesha vitendo hivyo, kwani kumekuwa na ugumu wa ushirikiano kati ya polisi na wananchi.
Aidha amewataka wananchi pamoja na viongozi wao kuweka mkakati wa pamoja katika ulinzi shirikishi.

Mwishoni mwa mwaka jana, waliuawa watu wa nane kwa kuchinjwa katika manispaa ya Bukoba, katika kipindi cha miezi miwili tu katika mwezi Novemba na Desemba 2014, ambapo polisi iliaidi kukomesha mauaji hayo, na kuwasihi wananchi kuachana na imani potofu. 

No comments:

Post a Comment