Ni mmiliki wa Jengo la kitega uchumi la kisasa lililo katika hatua za mwisho kufunguliwa Bw Naftari Felix ana kwea ana na camera yetu, Bw Nafu amesema ameamua kuweka kitega uchumi katika wilaya ya Muleba kwa sababu ya kusogeza huduma bora kwa wakazi wa Muleba na kutambua kwamba ni lazima sasa wazawa watambue kuleta m,aendeleo nyumbani. Jengo hilo lenye eneo la hotel, ukumbi mkubwa wa mikutano na shughuri mbalimbali,vyumba vya biashara mbalimbali,na Night club ya kisasa ambayo katika kanda ya ziwa itakuwa Muleba.Amesema huduma zote hizo zitazinduliwa rasmi tarehe 5-12-2014.Bw Nafu amesema siku ya ufunguzi anategemea kuzindua kwa stail ya aina yake kwani marafiki zake wapendwa wamemchangia kiasi cha shilingi milioni therasini kwa ajiri ya kumuunga mkono ,hivyo anatarajia kwenye ufunguzi kuwepo kiongozi mzito ambae hakumtaja jina ,ila amesema itakuwepo band kubwa ya hapa nchini itakayotoa burudani kwa wageni waalikwa, pia wasanii wa kubwa hapa nchini akiwemo Mrisho mpoto watatoa Burudani.Amesema baada ya shughuri za Ibada wakati wa asubuhi,jioni sherehe zitaendelea ikiwa ni pamoja na ufunguzi wa Night Club.
Ni muonekano kwa mbali baadhi ya majengo.
Kitega uchumi hiki kipo mkabala na jengo la NMB Muleba.
Sehemu ya maduka ya biashara.
Sehemu ya nje ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.
Ni jengo la aina yake kwa Muleba.
Sehemu ya ukumbi wa mikutano wakiendelea na matengenezo, utakuwa na uwezo wa watu 2000.
Matengenezo yakiendelea.
Sehemu ya Night club.
Matengenezo yakiendelea sehemu ya Night club.
Itakuwa ni Night club ya pekee kanda ya ziwa.
Eneo la hotel matengenezo yakiendelea.
Bw Nafu akifuatilia mafundi wanavyoendelea na kazi.
Ufunguzi rasmi ni tarehe 5-12-2014 Muleba .
No comments:
Post a Comment