Sunday 26 October 2014

MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KIISLAM 1436 KITAIFA WASHEREKEWA MKOANI KAGERA MANISPAA YA BUKOBA

 Waislamu kote duniani wamesherekea mwaka mpya wa kiislamu wa 1436,Kitaifa nchini Tanzania madhimisho ya mwaka mpya wa kiislamu yamefanyika Mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba na mgeni rasmi alikuwa Mufti wa Tanzania.
 Waumini wakiislamu wakiwa katika matembezi ya amani kusherekea mwaka mpya wa kiislamu mitaa mbalimbali ya Bukoba mjini.
 Matembezi ya amani kuelekea uwanja wa Uhuru Platform uswahilini Bukoba.
 Mufti wa Tanzania  ndio aliepokea matembezi ya amani.
 Shekhe Mustafa akiwasili viwanja vya Uhuru.
 Baba Askof Buberwa wa Kanisa la Kilutheri nae alishiriki sherehe za mwaka mpya wa kiislamu.
 Quruani tukufu ya ufunguzi wa sherehe ikisomwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanal mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na waislamu na kuwatakia heri ya mwaka wa kiislamu.
 Alhaj Ayub Kagera mwenyekiti wa Bakwata Bukoba Mjini.
 Mashekhe kutoka mikoa mbalimbali nchini na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini.
 Mkurugenzi wa Kasibante redio Richard Leo (kulia)akiwa na Yusuf Abed mtangazaji wakiwa Live Kasibante redio 88.5
 Channel 4 Tv wakichukua matukio.
 Ustadhi Chakindo.
 Kaswida wakitoa burudani.
 Dufu la Kansenene.
 Bi Sakina akifurahia dufu.
Ni dua ya kufunga sherehe mida ya saa saba usiku katika viwanja vya Uhuru platy form Bukoba.

No comments:

Post a Comment