Sunday 24 August 2014

KAKA MKUU ERNEST NYAMBO AAGWA KWA SHANGWE BUKOBA.

Keki tayari kwa Kuliwa usiku huu.Ernest Nyambo (kushoto) akiwa na rafiki yake Pedeshee Muganyizi kutoka kampuni ya Zachwa Investment kwenye sherehe ya kumuaga rafiki yake mpendwa Kaka mkuu. Mbele yao ni keki iliyoandaliwa vyema na ikiwa maalum kwa ajili ya kuliwa kwa ishara ya kumuaga ndugu yao ambaye amehamishwa kikazi kuelekea Jijini Dar es salaam.Naibu Kamishna George Kombe, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera (kushoto katikati ni RPC Mwaibambe Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera na kulia ni Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki wakiwa kwenye Sherehe ya kumuaga Ernest Nyambo ambaye amehamishiwa makazi Jijini Dar Es salaam kwa Kazi ya Kujenga Taifa.Shangwe za Sherehe ya kumuaga Kaka Ernest Nyambo zikiendelea..Bw. Ernest Nyambo akimlisha keki my wife wake kwenye sherehe ya kumuaga mumewe kipenzi iliyofanyikia kwenye Ukumbi wa Lina's Club Bukoba mjini usiku huu wa tarehe 23.08.2014 Mama Prisira Mwainunu nae alilishwa keki hiyoMama Prisira Mwainunu nae aligeuza kibao kwa Ernest Nyambo.Rafiki yake Jamali Kalumuna nae alilishwa keki na Ernest Nyambo
Marafiki wakishuhudiaKutoka Mwanza...kulia ni dada Anitha Z. akiwa na rafiki yake kwenye Sherehe ya kumuaga Kaka yao Ernest Nyambo.Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki(kushoto) akiteta jambo kwenye Sherehe ya kumuaga kaka Ernest Nyambo iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Lina's Club Bukoba.Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Umati wa Watu kwenye Sherehe hiyo iliyoudhuriwa na ndugu, Jamaa pamoja na Marafiki.
Ernest Nyambo alipata muda akaongea neno na marafiki zake ndugu na jamaa wa hapa Bukoba ambapo alikuwa akifanya kazi kwa muda mrefu kabla ya kuhamishwa kikazi kuelekea Jijini Dar es salaam. Ernest kwa Umakini wake na Utendaji kazi wake akiwa hapa Kagera ulimfanya achaguliwe katika nyanja mbalimbali alikuwa kiongozi wa Bukoba Veteran na pia  Kiongozi wa kikundi cha Wanaumoja cha hapa Kagera Uongozi ambao aliuendesha Vyema mpaka amehamishwa Kikazi na Ngazi hizo za Uongozi akiwaachia wenzake kuchukua nafasi hizo.

No comments:

Post a Comment