Sunday, 4 May 2014

NAWAULIZA WANA PAMOJA GROUP NANI MBADALA WA ERNEST NYAMBO BAADA YA KUJIUZURU UENYEKITI?

 Pichani  ni Bw Ernest Nyambo ambae siku ya tarehe 2-5-2014 alitangaza rasmi kujiuzuru nafasi ya mwenyekiti ya Umoja uliokuwa na nguvu kubwa katika Manispaa ya Bukoba (Pamoja Group)  pengine naweza kusema kuliko vyama vingi ambavyo vimekuwa vikiendesha shughuli zake kila mara na vya muda mrefu.   Binafsi napenda nieleze waziwazi kabisa kuwa taarifa hizi nimezipata leo kwa mstuko na majonzi makubwa maana natambua na kuelewa waziwazi kuwa huyu bwana alikuwa ni kiunganishi kikubwa sana katika umoja wetu na labda chini ya uongozi wake ndio maana tumeweza kuwepo na kufanya yale yote tuliyoyafanya.  Akiwa katika sherehe ya kumpongeza Mwanapamoja mwenzetu Bi RUKIA SIMBA MAWENYA katika ukumbi wa Lina's 2-5-2014 (sherehe ambayo sikubahatika kuwepo) Mimi JAMAL KALUMUNA mmiliki wa blog hii, Wageni wakiwa katika hali ya furaha kubwa na tukio la aina yake Bw SIMBA MAWENYA alimshangaza Mkewe Rukia pale alipoomba lango kuu la Linas's lifunguliwe ili aweze kuleta zawadi ya kumpongeza mke wake,Lango lilipofunguliwa watu walishuhudia Gari ya thamani ikiingia ukumbini(MORANO NISSAN) kitu ambacho kila aliekuwepo pale halipata mshangao na zaidi mke wake mpendwa Rukia alipobubujikwa na machozi ya mahaba ali akiwa haamini anachokiona mbele yake asilimia kubwa ya watu walitokwa na machozi ya furaha kila walipomtazama Rukia Mawenya akilia, hatimae zawadi ikakabidhiwa.    Baada ya muda mchache badae Bw Ernest Nyambo aliomba apewe nafasi ya kuongea na hasa kwa wanapamoja ambao katika ukumbi huo ndio walionekana kuwa wengi zaidi ya wengine.  Bw Ernest Nyambo akakabidhiwa kipaza sauti alianza kwa kuomba samahani kwa wageni waalikwa wote  kwa kile ambacho anataka kusema yawezekana wengine jambo hilo lisiwahusu ila aslimia kubwa  ya watu  walio hapa ni WANAPAMOJA hivyo kwa hili ninalotaka kuongea naona ni mahala pake, Bw Nyambo akasema kwa muda mrefu amekuwa Mwenyekiti wa umoja wa Pamoja tumeshirikiana kwa mengi, tumesaidiana kwa mengi, lakini katika farisafa ya kuachiana vijiti nimeona ni wakati muafaka sasa kuachia nafasi hii na kutoa mwanya kwa yeyote anaedhani anaweza kuitumikia nafasi hii, Nimeamua mwenyewe nikiwa sijalewa,sijachanganyikiwa, nina hakili zangu timamu na hakuna shinikizo lolote, Nawashukuruni nyote ambao tumeshirikiana katika kipindi changu chote cha uongozi. Mwisho wa kunukuu. lakini klabla hajamaliza akasema anamshukuru sana Salome(MAMA CHUI) ambae amekuwa msaada mkubwa katika umoja huu na mara nyingi ndio amekuwa akifanya kila kitu kwa niaba yake . hivyo akapendekeza wakati yeye ametoka na hakuna mwenyekiti akashauri Mama Chui ndio awe  Mwenyekiti wa muda mpaka hapo atakapopatikana Mwenyekiti. Hahika kila mtu alipokea kauli hiyo nzito kwa mshangao na stahili yake, wapo waliolia, wapo waliopagawa  na wapo waliosema bila utaratibu ili mradi kila mtu alionyesha kutokubaliana na maaamuzi ya Bw Nyambo.  Sitaki niongee mengi Wadau narudia kusema na kuuliza wana Pamoja sote tunajuana ni nani atakuwa na ustaimilivu wa kuwa na kifua cha kupokea, kusikiliza na kutoa majibu ya kumridhisha kila mmoja, ni nani kati yetu anaushawishi wa kushawishi jambo na kufanikiwa kwa muda mfupi? Nauliza Wanapamoja ni nani  wa kutoa kauli iliyosimama na kusimamia kauli yake? KIKUBWA KUMBUKA U moja wetu hauna katiba, hauna vikao vya wiki, mwezi au mwaka, umoja wetu hauna mfuko wa maafa, majanga wala matatizo , UMOJA WETU ulikuwa ni papo kwa papo kwa maana kwamba likitokea jambo  la majonzi au furaha muda wowote unaitwa na kinafanyika kitu kikubwa ambacho hata wenye vyama  vya kusaidiana vyenye katiba na makorokoro kibao hawawezi kufanya. Ndio maana nauliza Tunajuana nani wa kuchukua mikoba  ya Ernest Nyambo?    Wengi wetu ni wataalamu wa kuongea, kulaumu na fitina lakini hakuna msaada. Mimi namfahamu Nyambo ukiondoa swala la Pamoja nimekuwa nikimuona sehemu tofautitofauti akishirikiana na watu katika furaha na matatizo, lakini kikubwa anayo karama aliyopewa na mwenyezi mungu ya kuzungumza popote na kusikilizwa, karama hii ndugu zangu waliyonayo ni wachache duniani, wAWEZA UKAWA NA KILA KITU KWA MAANA YA MALI NA UWEZO MKUBWA ila watu wakakuchukia , au watu wasikusikilize, au watu wasitake uzungumze lolote, Lakini kwa huyu Bw Ernest nimekutana nae mayambohala pengi sana akiamasisha na kikubwa akifanikisha mambo mengi sana katika Manispaa yetu. Sina hakika ni nini kimepelekea AJIHUZURU lakini  binafsi nimepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa sana na kimsingi kama ningekuwepo katika sherehe hiyo ya kumpongeza Rukia ningekuwa miongoni mwa watu ambao nisingekubaliana na maamuzi hayo.SIOMBI IWE HIVYO lakini kwa namna ninavyojua umoja wetu WANAPAMOJA tumuombe sana mungu vinginevyo yawezekana ikawa ndio mwisho wa umoja huu. Najiuliza Nani wa kuvaa viatu vya Ernest Nyambo kukabidhiwa umoja ambao hauna katiba, umoja ambao hauna mfuko, umoja ambao hauna vikao, umoja ambao hauna ratiba ya vikao, umoja ambao ukipigiwa simu ni kutii na mengine mengi tu, nani ataweza?  NAWAACHIENI SWALI
 B W Ernest akiwa Bw Ramadhani kambuga na Bw  Mtensa hii ilikuwa ni moja ya shughuli ya kijamii
 Kila mahala anafika bila kujari Dini , ukabila, ubinafsi nk.
 Katika maswala ya  michezo
 Katika shuli za uamasishaji maendeleo  yupo
 Michezo ndio usisemeee
 Ni mikakati yake kila mahala
 Kwenye matatizo, misiba nk utamkuta
Bw Ernest Nyambo  najua maamuzi ya mtu si vizuri kuyaingilia ila binafsi bado nakuhitaji katika mambo mengi ya msingi, ya kuhakikisha tunasonga mbele si kurudi nyuma,mahala pengi umekuwa muhimili mkubwa na mambo yamekwenda.

No comments:

Post a Comment