Monday 23 December 2013

HAPPY BIRTHDAY JAMAL KABIGUMILA KALUMUNA (JAMCO)

Ni siku ya kumshukuru sana mwenyezi mungu mwingi wa rehema na upendo  mkubwa kwa viumbe wake, leo ni siku ya pekee katika maisha yangu, ni siku ambayo ilikuwa ni furaha kwa wazazi wangu Dauda Kalumuna na Khadija Elias Nasibu kwa  kumpata mtoto wa kiume, Nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunielea , kunisomesha na kunipa msingi wa maisha, Kipekee nitumie nafasi hii kumuombea mama yangu mzazi ambae ni marehemu mungu amlaze mahali pema peponi, Mama nilikupenda sana, nakukumbuka na kikubwa nazingatia uhusia na maelekezo yako yote kwa wadogo zangu, ndugu , jamaa , marafiki na Familia yangu,KWELI MUNGU NDIO KILA KITU, umenitendea mengi ambayo ni kama miujiza katika maisha yangu, Naishukuru kipekee familia yangu, wadogo zangu, jamaa wote na marafiki kwa msaada mkubwa walionipa  katika maisha yangu ya kila siku mpaka naifikia  tarehe ya leo 24-12-2013. asanteni sana.

No comments:

Post a Comment