Wednesday 12 August 2015

BALOZI KAGASHEKI APITISHWA KUGOMBEA UBUNGE CCM JIMBO LA BUKOBA MJINI, MKUTANO MKUBWA KUFANYIKA JUMAMOSI 15-8-2015 KUMTAMBULISHA MGOMBEA UBUNGE NA WAGOMBEA UDIWANI KATA ZOTE ZA JIMBO LA BUKOBA MJINI.

 Baada ya uzushi mwingi na upotoshwaji mkubwa uliokuwa umezaga katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bukoba, hatimae Uongozi wa juu kabisa wa chama cha mapinduzi Taifa umepitisha jina la Balozi Khamis Sued Kagasheki kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini kwa mara nyingine.Katibu wa ccm Bukoba mjini anapenda kuwatangazia wanachama wote, wapenzi wote na wananchi wote wa jimbo la Bukoba mjini kuwa tarehe 15-8-2015  siku ya jumamosi kuanzia saa 8.00 mchana katika uwanja wa Uhuru Platform utafanyika mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea udiwani kata zote 14 na mgombea ubunge.Mkutano huo utakuwa ni mkubwa na waina yake, utaanza na maandamano kutoka ofisi ya ccm wilaya mpaka uwanja wa Mayunga, Wananchi wote mnakaribishwa.
 Katibu wa ccm wilaya ya Bukoba mjini  Bw Gerrald Mwadallu anawakaribisha sana kwenye mkutano wa kihistoria katika jimbo la Bukoba mjini. 15-8-2015.
 Bw Anatory Aman miongoni mwa wagombaea 8 wa ccm ubunge kura hazikutosha.

Karibuni jumamosi 15-8-2015 KATIKA UWANJA WA UHURU PLATFORM,  NI KAZI NA DAWA, SHUGHULI PEVU,USINGOJE KUAMBIWA AU KUSIKIA UZUSHI UJE USHUHUDIE MWENYEWE,GARI KUBWA, MASHINE KUBWA,AIR FORCE ONE,KIFUBA KYA ITWAHWA(Imetolewa na katibu wa ccm Bukoba mjini.)

No comments:

Post a Comment