Saturday 16 July 2016

UMMY MWALIMU AZITAKA HOSPITAL TEULE ZA TAASISI ZA KIDINI KUWA MAKINI NA WAFANYAKAZI HEWA.

 Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi katika hospital teule za taasisi na masharika ya kidini ambayo wanapata ruzuku ya serikali kuwa makini na wafanyakazi hewa,Mh waziri Ummy ameyasema hayo katika mazungumzo na viongozi wa kidini katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa kagera kuwa serikali imekuwa ikitoa pesa nyingi kwa ajili ya mishahara, lakini cha kusikitisha pesa hizo zimekuwa zikilipwa kwa wafanyakazi hewa, ameongeza kwa kusema kuwa hata hao wafanyakazi hewa wamekuwa wakipokea kiasi kidogo ambacho akilingani na pesa iliyotolewa na serikali,Waziri Ummy amewataka kuwabaini wafanyakazi hewa wote, na serikali itakuwa ikilipa moja kwa moja mshahara kupitia kwenye account ya mfanyakazi na si kwenye account ya hospital kama ilivykuwa ikifanya awali.(katika picha waziri Ummy Mwalimu akizindua wodi ya wazazi iliyokarabatiwa na kuongezewa vyumba katika hospital ya Rufaa Mkoa wa Kagera.
 Kushoto Baba askofu Methodius Kilain akiwa na viongozi wengine zenye hospital kwenye taasisi za kidini.
 Kushoto ni mwenyekiti wa chadema Bukoba Manispaa, Bw Sherejei.
 Kushoto mkuu wa mkoa wa kagera meja jenerali Salum Kijuu.
 Mkuu wa mkoa wa kagera akisoma taarifa ya mkoa wa kagera.
 Hafla ya uzinduzi wa wodi ya wazazi hospital ya rufaa kagera baada ya ukurabati kukamilika.
 Mh Waziri akipita katika wodi ya wazazi.
 Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya hospital Joansen Rutabingwa akiwa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa kagera Costansia Buhiye.
 Mstahiki meya manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna.


1 comment: