Katika Ziara hiyo alitembelea kiwanda cha ndege cha Boeing na kupanga mikakati ambayo serikali ya awamu ya tano inatarajia kununua ndege mbili za kisasa ili kufufua shirika la air Tanzania ,pia alipata nafasi ya kutembelea Microsoft na kampuni ya Starbucks ambayo inaendesha migahawa mikubwa ya kahawa duniani. Balozi Huyo alimaliza mazungumzo yake kwa kukutana na Chama cha wafanyabiashara cha Seattle .
Ziara hizo ni moja mikakati ya serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika kupunguza matumizi ya serikali kusafirisha viongozi kutoka Tanzania kuja kufanya mazungumzo badala ya kutumia Mabalozi na wawakilishi waliopo kwenye nchi hizo
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa kwenye mkutano
na Watanzania Seattle jimbo la Washington nchini Marekani siku ya
Jumamosi July 16, 2016. Habari na Picha na Katunda Catunda Mwakilishi wa
Vijimambo Seattle, WA
katibu wa jumuiya ya watanzania Seattle (Tanzaseattle) Hajji Rajab Hajji akimkaribisha balozi
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiongea kwenye
mkutano na Watanzania Seattle jimbo la Washington nchini Marekani siku
ya Jumamosi July 16, 2016.
Wakati wa chakula.
Watanzania Seattle wakifuatilia mkutano na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi siku ya Jumamosi July 16, 2016.
Mkutano ukiendelea.
Watanzania Seattle wakimsikiliza katibu wa Jumuiya ya Watanzania Hajji Rajab Hajji alipokua akimkaribisha Mhe. Balozi.
Mkutano ukiendelea
hiyo Starbucks ailete kagera iwawezeshe wakulima wa kahawa
ReplyDelete