NI KIVUMBI!! "REDDS MISS LAKE ZONE 2013" JIJINI MWANZA UKUMBI WA GOLD CREST HOTEL USIKU WA LEO!!
Ni
kitimutimu cha Redd's Miss Lake Zone 2013 Kitakachofanyika leo Jijini
Mwanza 29-06-2013 katika ukumbi wa Gold Crest Hotel,warembo watatu
kutoka kila Mkoa katika mikoa sita ya kanda ya Ziwa watachuana kuwapata
watatu ambao watakwenda kwenye mashindano ya Taifa, mbali na mchuano
mkali utakaokuwepo, pia zitakuwepo burudani kutoka kwa Ommy Dimpoz na
Michael Ross. ili uweze kushuhudia mtanange huu kiingilio cha kawaida ni
Tsh20,000/= na VIP ni Tsh 40,000/=Washiriki wa redd's miss Lake zone 2013 wakifanya mazoezi yao ya mwisho leo kabla ya kuingia kwenye mtanange usiku huu. Kinyang’anyiro
cha kumpata Miss Kanda ya Ziwa kinatarajiwa kufanyika leo usiku katika
ukumbi wa Gold Crest Hotel uliopo jijini Mwanza. Mratibu wa Shindano
hilo Clara Mwassa, amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote
inayounda Kanda ya ziwa na kukaa kambini tangu Juni 23, Mwaka huu na
kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja leo hii Juni 29, Mwaka
huu baada ya Mshindi kupatikana.
No comments:
Post a Comment