Thursday 31 July 2014

REDD'S MISS KAGERA 2014 KUFANYIKA JUMAOSI 02, AUGUST 2014 KATIKA UKUMBI WA LINA'S CLUB

Warembo wakiwa kambini,katika pozi la picha ya pamoja.
Shindano la Redd's Miss kagera 2014, Linatarajiwa kufanyika jumamosi ya tarehe 02/08/2014 katika ukumbi wa Lina's Club.

Wednesday 30 July 2014

MIEMBENI FC WATINGA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA BAO 2-1 BILELE FC KWA DAKIKA 120!

Wachezaji wa timu zote mbili Miembeni Fc na Bilele Fc  wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza jioni hii.
Kikosi cha Timu ya Miembeni Fc
Kikosi cha Timu ya Bilele Fc
Mabingwa watetezi wa kombe la KAGASHEKI, Bilele Fc, wamefungwa leo na Timu ya Miembeni Fc bao 2-1 kwenye mtanange uliopigwa dakika 120, Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa  kutoshana nguvu kwa bao 1-1.
Timu ya Bilele Fc ndio walianza kupata bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 62 kupitia kwa Fikiri David na Miembeni Fc wakasawazisha bao hilo ndani ya dakika moja na Rashid Mandawa kupita katika dakika 63 baada ya mpira kuanza kati na kufanya shambulizi.
Dakika 90 zilimalizika na kwenda katika dakika za ziada na katika dakika ya 105 Miembeni walifanikiwa kupata bao la ushindi na mtanange kumalizika. Mtanange huu pia haukuweza kumalizika vyema kwani wachezaji wawili wa Miembeni Fc wameoneshwa kadi nyekundu 2 na kucheza pungufu katika dakika za mwishoni kwa kufanya makosa tofauti tofauti.
Ushindi huu unawapeleka  Miembeni Fc  hatua ya Fainali wakisubiri mshindi wa kesho kati ya Kitendaguro Fc na Kagondo Fc.
Bilele Fc wao wanasubiri atakayefungwa kesho kati ya Kitendaguro na Kagondo ili waje wakutane kutafuta mshindi wa tatu.Fikiri David wa timu ya Bilele Fc akimfunga kipawa Miembeni Samwel Geofrey kwa Mkwaju wa penati katika kipindi cha pili dakika ya 62.Fikiri David akishangilia bao lake mbele ya Mashabiki wao Nao Miembeni hawakupoteza nafasi walisawazisha bao hilo  ndani ya dakika chache moja na kufanya 1-1 katika kipindi hicho cha pili, Bao likifungwa na Rashid Mandawa.Kipa wa Miembeni akipangua mpira uliopigwa kwa kona.Wachezaji wa Bilele fc wakimdhibiti mchezaji wa Miembeni.Jesse Johansen wa Miembeni Fc akimkimbiza mchezaji wa Bilele fc Mohamed Nunda Mchezaji wa Miembeni Babu Seif (kushoto) akimtoka mchezaji wa Bilele fcKipa wa Miembeni fc Samwel akiwapanga wachezaji wake Frii kiki kuelekea lango la Miembeni fcKipa wa Miembeni Samwel Geofrey aliumia katika kipindi cha pili na mpira kusimama kwa mudaKipa wa Miembeni Samwel Geofrey akisimama na kuendelea kulinda lango lakePatashika langoni mwa timu ya Bilele FcKipa wa Miembeni samweli Geofrey akiokoa mpira wa kona langoni mwake Kipindi cha dakika za ziada 120 wachezaji wa Miembeni waliboresha ngome yao ili kulinda bao lao na hatimaye kuibuka na ushindi.Mashabiki wa Miembeni Fc wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 na kwenda hatua ya Fainali jioni hii.
Mashabiki wa Miembeni wakiwa wanawapongeza wachezaji wao baada ya kuwafunga Bingwa Mtetezi Bilele Fc na Ushindi huu kuwapeleka hatua ya Fainali.
Tunaenda Fainali!!! Mashabiki na Wachezaji wa Miembeni wakifurahia Ushindi huo!

PENATI ZAPIGWA TENA LEO KAITABA!! KITENDAGURO FC YAIBUKA BINGWA NA KUSONGA NUSU FAINALI!

Timu zote mbili kati ya Kitendaguro Fc na Rwamishenye Fc wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza
Kikosi cha Timu ya Rwamishenye Fc kilichoanzakikosi cha Timu ya Kitendaguro Fc (Makhirikhiri).
TIMU ya Kitendaguro Fc Maarufu kwa jina la Makhirikhiri wamewanyoosha wenzao nao wanaojulikana zaidi kama Wanabodaboda Rwamishenye Fc kwa Mikwaju ya penati 6-5 baada ya kutoshana nguvu katika dakika 90 ya bila kufungana! Mashabiki wa Timu mbili hizi kati ya Rwamishenye Fc na Kitendaguro walishindwa kuamini kile kilichotokea machoni mwao, Wakijionea kila timu ikishindwa kuliona lango la mwenzake huku kabla ya Mtanange kila mmoja alikuwa akijigamba kukwepa kwenda hatua ya Mikwaju ya penati! 
Mapema Kipindi cha kwanza hakuna aliyeliona lango la mwenzake katika dakika 45 za kipindi hicho nacho kipindi cha pili pamoja na Mtanange kushika kasi za mashabulizi ya hapa na pale timu zote zilibanana na kuweza kumaliza dakika 90 ya bila kufungana na Hatimae Mikwaju ya Penati kuamua nani wa kukamilisha timu nne za Nusu Fainali. Mikwaju ya Penati ilipigwa saba na hatimae Timu ya Rwamishenye kukosa 2 na Kitendaguro kukosa 1 hivyo Makhirikhiri kusonga hatua ya Nusu Fainali. 
Mashindano haya ya Ligi ya Kagasheki yataendelea hapo kesho kwa Nusu Fainali ya Kwanza kati ya Mabingwa watetezi Bilele Fc na Miembeni Fc.Kukaba ilikuwa ni mpango mzima Mchezaji wa Rwamishenye Fc Maximilian Thadeo (kushoto) akikabwa vilivyo na wachezaji wawili wa Kitendaguro Khamis na Timu kapteni Mchezo ulikuwa wa kasi sana katika kipindi cha kwanza kila mmoja akitaka kumwondoa mwenzake mapema.Mapema Mashabiki walikuwa wameishajichukulia nafasi zao katika Uwanja wa Kaitaba si Jukwaa kuu wala majukwaa madogo..saa tisa kamili nyomi ilishashona!!!Mambo ya Mizuka ya ligi hii ya Kagasheki 2014, Leo hata Vuvuzela zilipigwa!Nyomi ya Mashabiki Jukwaa Dogo!Mashabiki Wakina Mama nao hawakuwa nyuma!! Leo ndani ya Kaitaba!Viongozi wa Timu ya Kagera Suagar ya Hapa Bukoba nao walikuwepo kaitaba Uwanjani!! katikati noi Kocha Msaidizi wa Timu ya Kagera Sugar inayoshiriki Ligi kuu Vodocom na kulia ni Bw. Mwamed.Khamis (kulia) wa Timu ya Kitendaguro akipanga amtoke vipi Straika wa Rwamishenya Edwin Issack(kushoto) katika kipindi cha kwana.Seleman Khamis wa Rwamishenye akifanya mashambulizi Mwisho wa yote alikutana na ngome kali ya beki wa Kitendaguro safari ikaishia hapo!Seleman Hamis alisumbua sana ngome ya KitendaguroHapa sasa hutoki!!Mbele ya Mwamuzi vijana wakichuana huku Mwamuzi akiwasoma!Rwamishenye waliotea bao hapa na Mwamuzi wa pembeni akawapiga kibendera!Mashabiki wa Rwamishenye wamekosa nafasi wakaamua Bodaboda zao kuwa sehemu ya kiti!Dakika 90 tuazimaliza hivi hivi !! ndio maana tunaitwa Wanabodaboda wa Rwamishenye!!Mashabiki leo waliingia kwa Wingi kushuhudia Kipute nani anahitimisha nafasi ya Nne kwenda Nusu fainali.Mikwaju ndio iliwatoa Rwamishenye na hapa ni kipa wake akipelekeshwa katika mkwaju wa Mwisho!! mpira umepigwa huku yeye akajitupa kule!!Wachezaji wa Kitendanguro wakishangilia kwenda Nusu Fainali baada ya kuwatoa kamasi Wanabodaboda timu ya Rwamishenye Fc penati 6-5kushoto ni kipa wa Makhirikhiri Kitendaguro Fc akifurahia ushindi na mwenzakeUshindi Mtamu!!! tunaenda Nusu Fainali!!!Dada Shabiki wa Timu ya Kitendaguro alishindwa kujizuia akajikuta katikati ya Uwanja!!