Saturday 11 May 2013

HEKARU LA PROFESA ANNA TIBAIJUKA LILOJENGWA KATIKA SHAMBA LA MIGOMBA MULEBA

            Si jina geni masikioni mwako ukisikia jina la profesa Anna Tibaijuka,kila mmoja ananamna anavyomtambua,kwa ufupi ni mama makini mchapakazi anapokuwa kazini,Profesa anna ni mbunge wa muleba kusini,lakini pia ni miongoni mwa wabunge wachache waliobahatika kupata uwaziri katika serikari ya awamu ya nne ya rais jakaya kikwete,                            Nikiwa katika mizunguko yangu ya kutafuta riziki nilijikuta nakutana shamba zuri la migomba ,lakini kilichonivuta zaidi mpaka kuwa na shauku ya kusogea karibu ni uzio wa asili uliokuwa unazunguka shamba hilo,nilijikuta nataka nikaribie eneo hilo kwa karibu ili nionejinsi uzio huu ulivyotengenezwa kwa kutumia majamvi maarufu kama(ebilago au enshero)nikasogea kwa karibu zaidi,nilipofika getini nilichungulia kwa ndani ndo nikakutana na kitu kinaitwa hekaru lililojengwa migombani,nikazidi kusogea mafundi walikuwa wapo busy,nilimuhita mmoja wapo ili nijue mmliki wa bangaloo hilo,ndo nikaelezwa ni la profesa ANNA TIBAIJUKA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI.  SIKUSTUKA,kwa sababu nilianzia kufikiri enzi akiwa mwanaharakati,akapata wadhifa umoja wa mataifa UN HABITAT ,tena nafasi nyeti,katoka huko mojakwa moja kawa mbunge na hatimae waziri nikaona anastaili hekaru kama ili kuliweka migombani.
 Hata angekuwa wewe ungetamani kusogea karibu kujua kwenye uzio huu kuna nini.

 Sehemu ya mbele ya kuingilia,angalia geti la mbao linavyoendana na majamvi ya uzio
 Nikasogea taratibu nikakutana na kitu ,usipime na muleba migombani

 Kitu hicho cha profesa Anna Tibaijuka,ndo kinamaliziwa uwanja wa nje, ndani tayari kimeisha

 Sehemu ya juu, unaangalia chini,upepo mwanana na mandhali ya green usipime,muleba inatisha.


 Sehemu ya chini ya hekaru la profesa Anna Tibaijuka,lililopo muleba

 Kuna kitu cha msingi sana katika hekaru hili kuna njia ya walemavu wa viungo,wanasehemu yao ya kupita



 Jumba hili kwa hakika ni zuri na ni staili ya mama Anna Tibaijuka

 kwa mbele zimeanikwa kahawa,pamoja uaziri kilimo kinaendelea

           Pongezi sana mama Anna Tibaijuka, umejiandalia mazingira mazuri ya kuishi,wengi wao wangependa hekaru kama hili mtu analijenga mjini kwa maana ya biashara au kuishi,wewe umelijenga kagera,tena muleba migombani.ongera mama.                                                                                     

CAMERA YETU MULEBA


Kwa wale wanaoijua muleba miaka ya tisini ni tofauti na ilivyo sasa,muleba barabara kuu ni lami,lakini pia huduma muhimu zote utazipata,lakini pia akina mama hawako nyuma katika utafuta wa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali,camera yetu katika pitapita tulijikuta tunakutana na wamama wachapa kazi,wakiwa katika maeneo yao ya kazi,aliesimama na shamila seif na kulia kwake alijitambulisha kwa jina la mama dani

Mama dani akiwa anaonekana mwenye furaha,mama anaejishughulisha anaishi muleba na ameridhika na maisha yake si tegemezi

Nilipita pita mitaani nikakutana ukumbi wa disco ,nikajua hapa baada ya kazi watu wanaburudika

Ukitaka kuujua mji watu wake ni waelewa kiasi gani ,kuna vitu vya msingi uvipate

Na mahala kama ni pazuri watu watakuja kutembea tu,camera yetu ikakutana na ngudu haruna akiwa na hamimu,mzuzu kwa sana we acha tu.....


Nakwambia muleba si mchezo,hawako nyuma katika maswala ya kwenda na wakati,ngugu kamanzi anaendelea na kazi za video,picha,editing ,tena kwa kutumia vifaa vya kisasa,muleba asikwambie mtu wako juu.

Bwana majura akiwa ofisini,miaka ya nyuma ameishi bukoba mjini akiwa benny bazary ,baadae akaamua kuamia muleba,ndio maendeleo watu wanang'ang'ania mijini wakate unaweza kwenda popote na maisha yakaenda.

muleba kumekucha


Muleba town tukakuta watu wako busy,hii inakupa picha mji unakuwa kwa kasi


ukiwa Muleba unapata huduma za mitandao yote,kwa maana ya mawasiliano na pesa kwa mtandao

Kumbi za sherehe,mikutano nk si tatizo Muleba ,camera yetu moja kwa moja ukumbi wa waisuka,ni ukumbi mkubwa unaoweza kuimili idadi ya watu zaidi ya 1000,na hapa ndo inafanyika REDD'S MISS MULEBA 2013 SIKU YA TAREHE 31-5-2013 IJUMAA,DAYNA NYANGE ATATOA BURUDANI NA WASANII WENGINE KIBAO.


HAPOHAPO WAISUKA IPO NIGHT CLUB KAMA UNAVYOIONA INAPENDEZA ,DISCO KILA IJUMAA,JUMAMOSI NA JUMAPILI,HIYO MULEBA


MULEBA KUMEKUCHA JAMANI

USIKOSE REDD'S MISS MULEBA 31-5-2013 WAISUKA MULEBA

MALAZI KWA MULEBA SI TATIZO TENA HOTEL ZA UKWELI

DUKA HILI LIPO MIGOMBANI KABISA ,HII INAKUPA PICHA MULEBA MAENDELEO NI MAKUBWA

HAPA NDO NILICHOKA MABOMBA MPAKA MIGOMBANI, MAMA NA MTOTO WANACHOTA MAJI,KWA STAILI HII VIJIJINI WATU WATAISHI MAANA MAENEO MENGI MAJI NI TATIZO ILA MULEBA WANASONGA MBELE


NI HOTEL MPYA HIYO INAJENGWA MULEBA YA NDUGU OCTAVIANI MUTALEMWA ANAISHI DAR ILA MAENDELEO ANALETA NYUMBANI NI MFANO WA KUIGWA

NIKAPITA MTAA MMOJA HIVI NIKAKUTANA NA MTAMBO WA KUKAMATA SENENE,MULEBA SI MCHEZO


UKITAKA KUJUA MJI UNAKUWA NI HUDUMA KAMA HIZI KUWEPO,WATU WA KUTOA PESA ILI WATU WAFANYE KAZI WAZALISHE KWA KUWEZESHWA MIKOPO KAMA HIVI ,JAMAA HAWA MULEBA WAPO.


MAJUMBA MAZURI WATU WANAJENGA,MULEBA INAPENDEZA

STAND YA MULEBA HIYO


UKIFIKA MULEBA MJINI DIWANI WA PALE ANAITWA HASSAN MILINGA KWA TIKETI YA CUF, NA MBUNGE WA HAPO NI MAMA ANNA TIBAIJUKA HUPO HAPO ILA KAZI ZINAKWENDA JAMANI.

KIKUBWA MAENDWLEO ITIKADI ZA VYAMA PEMBENI,NDO MPANGO MZIMA



ASIKWAMBIE MTU MULEBA NGOZI HII NDO MAHALA PAKE


WATU WANACHAPA KAZI MULEBA


STAND WATU WANASUBIRI USAFIRI ,MULEBA HIYO


NAKWAMBIA MULEBA JAMANI mmmm

JR SERVICE STATION WAUZAJI WA MAFUTA MULEBA,MJI UNAKUA KITUO CHA KISASA,ONGERA BWANA RWEYEMAMU

JR SERVICE STATION MULEBA WAKISHUSHA MZIGO

WAKATI NARUDI BUKOBA MJINI NIMEFIKA MAENEO YA KAGOMA NIKAKUTANA NA MAAJABU,HUYU MTU KAFUNGA MBO KWENYE PIKIPIKI HEBU JIULIZE KAMA GARI LINAKUJA KWA MBELE YAKE NA NYUMA YAKE LIKO GARI KAMA HIVYO NINI KINAWEZA KUTOKEA, NINA HAKIKA MSOMAJI MAJIBU UNAYO NI AJALI,SASA MIMI NILIAMUA KUSIMAMA ILI KUMUELIMISHA KIJANA HUYU,ILA KATIKA GARI LANGU NILIKUWA NIMEMPA LIFTI MWANAJESHI ,HIVYO TULIPOSIMAMA TU KIJANA ALIGEUZA PIKIPIKI KWA NGUVU BAABA YA KUMUONA MWANAJESHI NA KUTOKA MKUKU KAMA UNANYOONA PICHA YA CHINI

HUYO ALITOKA MKUKU

WATU KAMA HAWA NI TATIZO KATIKA JAMII,JAMANI BADILIKENI MADERAVA PIKIPIKI

TUKAFIKA MUHUTWE,SI UNAJUA PALE NANASI,MACHUNGWA, NA MACHENZA KWA WINGI ,NA WP NILIEMPA LIFT AKASHUKA KUNUNUA MATUNDA


KIMSINGI KWA LEO NDIO SAFARI YANGU ILIVYOKUWA,KIKUBWA MULEBA INAKUWA KWA KASI, KINACHOFUATA MPENDWA NAKULETEA HABARI YA MAMA ANNA TIBAIJUKA USIKOSE KUANGALIA jamcobk.blogspot.com kwa habari za uhakika tupigie simu namba 0788-707027,0754-757157 au 0714-707027,tunaanza mchakato wa matangazo,karibu utangaze nasi.