





Katikati ni Super Nyota Divas, Joylen Aliyeshinda katika katika shindano la kumtafuta msanii wa kike kupitia Mikoa yote inayopita Fiesta, Shindano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Lina's Club.
Joylen aliwashinda wenzake kwa kila vigezo vilivyokuwa vikiangaliwa na Majaji. Joylen amekuwa akiimba nyimbo za Recho na Vumilia ikiwemo, Nashukuru umerudi, Upepo wako na zinginezo.
Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group, Ruge Mutahaba (kulia, akiwapongeza washindi wa BK Dancers waliojinyakulia Millioni moja.
Msanii wa Muziki Ras Nod wa hapa Bukoba akiwajibika kuwaburudisha mashabiki wake jukwaani
Sehemu ya umati wa wakazi wa Mji wa Bukoba na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Tamasha la Serengeti fiesta 2014 katika Uwanja wa Kaitaba leo
Msanii wa Hapa Ntymbani Bukoba Nshomile akiimba mbele ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Kaitaba wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Fiesta 2014, Tamasha lililofanyika kwa mara ya kwanza katika Mkoa huu wa Kagera na kushuhudiwa na Wakazi wengi wa Mji huu na Vitongoji vyake.
Nshomile Family akiutendea haki wimbo wake!
Wadau na Vinywaji vyao aina ya Serengeti wakifuatilia kwa karibu Tamasha hilo huku wakifurahia jambo kwenye Uwanja wa Kaitaba ambako ndipo Tamasha hilo limefanyikia leo ijumaa.
Msanii mkongwe wa nyimbo za asili ya Kihaya Nchini mwenye sauti ya aina yake Saida Karoli akiwa na Kundi lake zima wakipagawisha Wakaazi wa Bukoba leo kwenye Tamasha la Fiesta 2014 Mjini Bukoba.
Saida Karoli akicharaza ngoma tatu kwa mpigo na kuwashangaza Mashabiki wake.
Ngoma ikishika kasi jukwaani!!
Saida Karoli akikonga nyoyo za umati wa Wakazi wa Mji wa Bukoba waliojitokeza katika Uwanja wa Kaitaba katika tamasha la Serengeti fiesta 2014.
Kundi zima la Saida Karoli likijiachia kwa nyimbo za Asili jukwaani
Saida Karoli akifanya yake Jukwaani..
Nyomi...
Mikono juu!!!
Simu nazo zikawa Viganjani juu kwa juu!! Kuamsha Fiesta!!! Upendo nao ukisambazwa kitaratiiibu!
Hakika ilikuwa ni Sheeeeda!!!
Hii ni Historia Bukobaaaa!!!
Willy O. Rutta yakamshinda...akabaki hana hili wala lile!! Zote ni Shangwe na Furaha za Fiesta 2014 Bukoba Usikuu huu...
Sambaza upendo na hamsha hamsha za hapa na pale!
Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Recho akifanya yake jukwaani!!
Msanii wa Bongoflava Jux nae aliwajibika kisawasawa jukwaani
Mikono juu!! 


Linah na waimbaji wake wakifanya yao kwenye Usiku wa Fiesta
Linah akipawawisha Mashabiki wake
Msanii wa Bongoflava Barnabas
Barnaba akiwapandisha kwa hamsha hamsha mashabiki wake katika Tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba na kushuhudiwa na Maelfu ya Watu.
Tamasha ili la Fiesta lilikuwa ni la kwanza hapa Bukoba tangu yazinduliwe hapa Nchini Tanzania..
Barnaba akiendelea na Kuburudisha kwa nyimbo tofauti tofauti katika Tamasha hilo Mjini Bukoba.
Dada alishindwa kuvumilia!! Furaha ilimteka kwa Barnabas
Msanii wa bongofleva Mr. Blue
Bk Sande akishambulia Jukwaa!

Msanii wa bongofleva anaekuja kwa kasi katika mchakato wa kuchanganya nyimbo za asili na za kizazi kipya kutoka hapa hapa Bukoba, BK Sande akiimba baadhi ya nyimbo zake Mbele ya Maelfu ya wakaazi wa Mji wa Bukoba katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014
Msanii wa bongofleva wa Bukoba, BK Sande akiimba kuwabueudisha Wahaya wenzake kwa miondoko ya Kihaya zaidi...nyumbani ni Nyumbani!
Msanii wa Bongoflava Ommy Dimpoz ulifika Muda wake..
Kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika Bukoba...salaam kutoka kwa wadau wake ilikuwa mhimu sana
Ommy Dimpoz
Nipe tano..!
Alikuwa na wenzake Jukwaani na walikuwa na staili ya aina yao kuichezaji!
Ommy Dimpoz akicheza na Vijana wake kwa staili yao ya kipekee!
Ommy Dimpoz akiendesha kamuzi la aina yake jukwaani
Ney wa Mitego jukwaani
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ney wa Mitego akiimba moja ya nyimbo zake katika Tamasha la Fiesta 2014 katika Uwanja wa Ksitaba.


Dj Fetty na wewe Unaimba??
Dj Fetty nae ilikuwa siku yake ya kwanza kufika Bukoba...hivyo na yeye alijikusanyia mashabiki wake akiwa jukwaani....Furaha yake alijikuta anacheza na kuongea maneno machache na Wakaazi wa Bukoba akiwa jukwaani Wakati Tamasha la Fiesta likiendelea katika Uwanja wa Kaitaba..!
Dj Fetty akiachia 1,2...jukwaani.

Willy O. Rutta akiteta jambo na Ruge Mutahaba
























































