Tuesday 16 January 2018

THE MINT CLUB KUFUNGULIWA 19-1-2018 IJUMAA, BUKOBA KUMEKUCHA...

 Kile kilio cha muda mrefu kwa watu wa Bukoba na Kagera kwa ujumla kukosa Club ya maana, sasa Ndugu Muganyizi Zachwa mfanyabiashara maarufu Bukoba anamaliza kilio hicho ,baada ya kukamilisha ujenzi club kubwa na ya aina yake itakayofunguliwa siku ya ijumaa 19-1-2018itakojulikana kwa jina la The Mint Club.Club hiyo ambayo ipo katika barabara ya Kashozi  Bukoba mjini katika jengo maarufu la Rwabizi ghorofa ya kwanza itafunguliwa na mmoja wa kiongozi wa serikali ambae jina litatangazwa hapo badae,DJ Ommy Crazy,Rose Ndauka na wengine watakuwepo, The Mint club ni miongoni mwa club kubwa Tanzania yenye muonekano wa kisasa na vifaa vya kisasa, vinavyoendana na kasi ya teknologia ya kisasa,mbali na hudumu ya muziki pia itapatikana huduma ya chakula, vinywaji na malazi katika ghorofa ya pili,takribani watu zaidi ya arobaini watapata ajira.
 Muonekano eneo la vip.
 Maeneo ya kawaida.
 Sehemu ya Dj.
 Vifaa vya kisasa.
 Muonekano wa mataa na spika.
 Muonekano wa kaunter.
 Wadada watakaotoa huduma.
 Sehemu ya VIP.
HII SI YA KUKOSA, UFUNGUZI WA THE MINT CLUB 19-1-2018, DJ OMMY CRAZY ATAKUWEPO , WATU MAARUFU KAMA AKINA ROSE NDAUKA NA WENGINE WATAKUWEPO.

Sunday 14 January 2018

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye Gadi ya Jeshi ya heshma pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili (hazionekani pichani ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.