Saturday, 6 July 2013
MICHUANO YA KOMBE LA KAGASHEKI YAANZA LEO HII KWENYE UWANJA WA KAITABA BUKOBA. TIMU YA HAMUGEMBE IKITANDIKWA NA BAKOBA BAO 1-0
MAGUFULI AUTAMANI URAIS 2015
![]() |
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli,
anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi
masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya. Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho. Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali. Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015. Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo. Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge. |
Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.
“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.
“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.
Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.
Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Friday, 5 July 2013
NDOYA YA DIAMOND NA PENNY IMEIVA
![]() |
Diamond & Penny |
SIYO siri
kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny
Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni
namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku
ikifika.
Akizungumza na
gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno
ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye
maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na
mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
“Suala la ndoa
yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila
wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa
yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia
kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi (10,000). Itakuwa ni ndoa
ya Wasafi bana,” alisema Diamond.
RAIS KIKWETE KUWA REFA TAMASHA LA MATUMAINI
MA PETRONIDA MPILLA HATIMAE AFIKISHA MIAKA 60 YA UTUMISHI WA UMMA ,APONGEZWA NA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA MKOA,WANAWE,WAJUKUU, NDUGU NA MARAFIKI
Ni siku ya historia katika maisha ya ma Petronida mpilla kustaafu kazi salama akiwa mtumishi wa serikali,ma petronida amitimiza miaka 60 akiwa kazini na sasa amestaafu,katika kipindi chote cha utumishi amekuwa akifanya kazi katika hospitali ya mkoa wa kagera na mpaka anastaafu alikuwa amefikia cheo cha daktari,katika kutoa shukrani katika sherehe ya kumpongeza amewashukuru wafanyakazi wote ambao amekuwa nao kwa kipindi chote cha utumishi wake,ma petronida mpilla akiwa na furaha aliwasimamisha wanae na wajukuu ukumbini hapo ili wageni waalikwa waweze kuwatambua, Ma petronida sasa amestaafu rasmi.
ma petronida akiingia ukumbini
wajukuu wa ma petronida wakijiandaa kuingia ukumbini
wajukuu wakiingia ukumbini kwa kucheza kumpongeza bibi yao
chezeaa wajukuu weweee
ni wakati wa keki
mjukuu khadija jamal katokelezea
bibi petronida akiwasha mshumaa
maelekezo ni muhimu kutoka kwa mwanae jamira jamal (kushoto)
keki ikakatwa
mdogo mtu nae akawajibika kwa dada
wageni wakifuatilia matukio
wajukuu wakilishwa keki na bibi
ukafika wakati wajukuu na watoto wakaonyesha ujuzi katika kusakata rumba usiombee ilikuwa ni balaaaaaa
ashura ashiraf nae ndani ya nyumba
watoto wa ma peto hawa ni mapacha awaachani hata ukumbini ni benet
ikafika wakati ikapingwa ngoma
u wakaruka juu na kushuka
ni vijimambo tu katika ngoma
ma peto akasalimia wageni wote na kuwashukuru kwa kufika
mapozzzzz
watoto wa ma peto nao wakaselebuka ,nakwambia ilikuwa rahaaa
daktari mfawidhi akatoa neno
wajukuu wakaibuka na zawadi ya bibi
watoto wakaibuka na friji
mama akakabidhiwa jokofu
wakwe nao wakazuka,jiko la gesi na pochi zikatolewa
wageni waalikwa nao wakaja kutoa zawadi
misosi time
yazidi( mkwe)
picha ya pamoja,watoto,ndugu na jamaa
mapozzzz
ongera mama
ongera sana mama
dah wajukuu vituko vingi
mama jamcobukoba.blogspot.com tunakupongeza kwa kuitumikia serikali na jamii katika utumishi uliotukuka wa miaka 60,mungu akuongoze katika maisha yako mapya katika jamii na hasa hapo nyumbani kitendaguro,ongera sana
ma petronida akiingia ukumbini
wajukuu wa ma petronida wakijiandaa kuingia ukumbini
wajukuu wakiingia ukumbini kwa kucheza kumpongeza bibi yao
chezeaa wajukuu weweee
ni wakati wa keki
mjukuu khadija jamal katokelezea
bibi petronida akiwasha mshumaa
maelekezo ni muhimu kutoka kwa mwanae jamira jamal (kushoto)
keki ikakatwa
mdogo mtu nae akawajibika kwa dada
wageni wakifuatilia matukio
wajukuu wakilishwa keki na bibi
ukafika wakati wajukuu na watoto wakaonyesha ujuzi katika kusakata rumba usiombee ilikuwa ni balaaaaaa
ashura ashiraf nae ndani ya nyumba
watoto wa ma peto hawa ni mapacha awaachani hata ukumbini ni benet
ikafika wakati ikapingwa ngoma
u wakaruka juu na kushuka
ni vijimambo tu katika ngoma
ma peto akasalimia wageni wote na kuwashukuru kwa kufika
mapozzzzz
watoto wa ma peto nao wakaselebuka ,nakwambia ilikuwa rahaaa
daktari mfawidhi akatoa neno
wajukuu wakaibuka na zawadi ya bibi
watoto wakaibuka na friji
mama akakabidhiwa jokofu
wakwe nao wakazuka,jiko la gesi na pochi zikatolewa
wageni waalikwa nao wakaja kutoa zawadi
misosi time
yazidi( mkwe)
picha ya pamoja,watoto,ndugu na jamaa
mapozzzz
ongera mama
ongera sana mama
dah wajukuu vituko vingi
mama jamcobukoba.blogspot.com tunakupongeza kwa kuitumikia serikali na jamii katika utumishi uliotukuka wa miaka 60,mungu akuongoze katika maisha yako mapya katika jamii na hasa hapo nyumbani kitendaguro,ongera sana
Subscribe to:
Posts (Atom)