Friday 28 March 2014

CAMERA YETU PANDE ZA HAMUGEMBE LEO DARAJA LA KANONI,NI MWEZI MMOJA NA SIKU CHACHE TANGU LIFUNGULIWE BAADA YA UKARABATI KUKAMILIKA NA KUTUMIA ZAIDI YA MILIONI 300 NA SASA LINAFANYIWA TENA

 Nakumbuka siku hiyo takribani mwezi moja na siku kadhaa zimepita maeneo ya daraja hili la Kanoni barabara kuu inayounganisha manispaa ya Bukoba na  Mikoa mingine ilikuwa ni furaha, nderemo na vifijo, huku wananchi chini ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Fabian Massawe wakishuhudia kwa macho na taarifa iliyojaa matumaini na weredi mkubwa kuhusu ukamilishaji wa ukarabati wa daraja hili la Kanoni. Kipindi hicho daraja hili lilipofungwa ilitokea adha kubwa kwa magari kupitia njia zingine ambazo zilisababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi ,lakini pia kwa madereva na kusababisha ajali na watu kupoteza maisha.Kwa taarifa iliyotolewa siku hiyo kwa mbwembwe na umaili mkubwa mbele ya mkuu wa mkoa kwa kutumia mamilioni ya fedha, leo ndani ya mwezi mmoja na siku  hali iko hivi.Hapa yapo maswali ya msingi sana kujiuliza ,Lakini kikubwa ni watu kutambua kuwa wale waliobahatika kupewa dhanana ya kusimamia masrahi ya watu watambue pia wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi, na zaidi ya hapo waende mbali zaidi kuwa Duniani  tunapita na kila kilichomo, ulichonacho , ulichokula, ulichokipata aidha kwa haki au vyoyote vile utaviacha na utahukumiwa kulingana na matendo yako.
 Ni  swala la kusubiri, maana hata pikipiki haiwezi kupishana na gari kutokana na ufinyo wa daraja kwa sasa
 Ni msongamano wa magari ambayo inabidi  yasubiri
 Hili ndio daraja ambalo upande mmoja  linafanyiwa ukarabati tena, na hali hii kusababisha msongamano

Thursday 27 March 2014

UTIMIZA MIAKA 3 YA KLABU YA BONGO MOVIE ITAKAYOFANYIKA MEI 2


 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade house Mikocheni.
 Steve Nyerere akinadi kinywaji cha Windhoek ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movies, Sherehe itakayofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni jijini Dar Es Salaam Ijumaa ya tarehe 28.
Rais wa FM Academia Nyoshi Ali Sadat akiongea na wadau waliofika katika ukumbi wa East 24 wakati wa utambulisho wa wasanii na bendi zitakazotoa Burudani siku ya Sherehe ya Kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie itakayofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House ijumaa ya tarehe 28 Mwezi huu
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mabibo Beer, Bw Jerome Rugemalila akiongea na Waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa Bendi na wasanii watakaotoa burudani ya nguvu siku ya sherehe ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie itakayofanyika tarehe 28 katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni Jijini Dar.
 Baadhi ya wasaniii wa Bongo Movies wakifuatilia kwa makini 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Benadetha Rugemalira (aliyeshika kinywaji cha Climax) akifuatilia kwa makini matukio wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani siku ya ijumaa kwenye sherehe ya Kuazimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie
 Baadhi ya wadau waliohudhuria utambulisho huo uliofanyika katika ukumbi  wa East 24
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalira (kulia) akijadiliana jambo na Meneja masoko wa Mabibo Beer, Jerome Rugemalira (pili kulia) na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bwa Steve Nyerere na Msanii wa bongo movie Adam Kuambiana
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akijadiliana jambo na Katibu wa Bongo Movie Mtitu wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani wakati wa sherehe za kutimiza miaka mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.

RIDHIWANI AENDELEA NA KAMPENI BWILINGU


 Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Matuli Kata ya Bwilingu na kuwaambia CCM ni Chama pekee kinachoweza kuahidi na kutekeleza yale yalioahidiwa.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Martine Shigela  wakati wa mkutano wa kampeni za CCM kijiji cha Matuli kata ya Bwilingu.
 Mgombea Ubunge jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wakina mama wa kimasai waliokuja kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kijiji cha Matuli.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Nsugu Ridhiwani Kikwete akipandisha bendera baada ya kufungua shina la wakereketwa  la Msimamo.
 Msanii maarufu Dokiii akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakina Mama wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge kupitia CCM kwenye kijiji cha Matuli
 Msanii Hafsa Kizinja akitumbuiza huku mgombea wa Ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kijiji cha Matuli.

Wednesday 26 March 2014

YALE MANENO YA KUFA KUFAANA YAMETIMIA UWANJA WA KAITABA BUKOBA KUFUATI UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2-5-2014

  Wa kale walinena  Kufa kufaana, maneno haya yametimia na kuleta faraja kwa wakazi wa manispaa ya Bukoba na Mkoa mzima wa Kagera kufuati ujio wa mbio za mwenge kitaifa zitakazozinduliwa rasmi 2-5-2014 katika uwanja wa Kaitaba.Yamekuwepo malalamiko ya muda mrefu sana kwa wapenzi wa soka kulalamikia ubovu wa majukwaa na miundo mbinu mbalimbali katika uwanja huu,Lakini kufuatia  tukio la uzinduzi wa mbio za mwenge yapo marekebisho makubwa yanaendelea katika uwanja huu, na Leo 26-3-2014 Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Kanal Fabian Masawe alifika kujionea hali halizi ya maendeleo ya marekebisho ya uwanja nas kujionea  Wanafunzi  mia sita wa Halaiki wanaoendelea na mafunzo mbalimbali ya gwaride na nyimbo kwa ajili ya uzinduzi wa mbio za mwende Kitaifa Mkoani Kagera.
 Ni moja ya jukwaa ambalo linatengenezwa na litaezekwa juu kwa bati kumuwezesha mkaaji asipigwe na jua au kunyeshewa na mvua, na mbao zake zikiwa zimewekwa imara zaidi,
 Ukarabati ukiendelea
 Wanafunzi  mia sita wa shule za msingi katika baadhi ya shule Manispaa ya Bukoba wakiwa katika mafunzo ya Halaiki
 Kushoto ni Afisa Elimu shule za msingi Manispaa ya Bukoba Ndugu Fande akiwa na Afisa Utamaduni Manispaa Ndugu Rugeiyamu wakiratibu shughuli zote katika uwanja waKaitaba

 Ni Nesi akitoa huduma kwa wanafunzi wenye matatizo mbalimbali wanaoendelea na mafunzo ya Halaiki
 Muonekano wa Jukwaa

 Mkuu wa Mkoa Kagera Kanal Fabian Massawe akisalimiana na walimu wanaendelea kusimamia na kufundisha mafunza ya Halaiki wanafunzi
 Mwl J J Mugango(kulia) ni miongoni mwa walimu wanaofundisha na kushoto ni Ndugu Kilema Athuman Kambagwa mkufunzi wa Halaiki
 Mwl Alistidia ambae ni katibu  mkufunzi akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa
 Wanafunzi katika pozz tofauti
 Utapenda , vijana wanaweza
 Ni miongoni mwa alama ambazo wanafunzi wanafundishwa na wataonekana hivi
 Mwalimu anapokuwa kazini hakuna mchezo
 Ni manjonjo ya kila aina wanafunzi wa Halaiki haoo
 Hii ndio timu nzima

 Afisa utamaduni akimkaribisha Mkuu wa mkoa aongee na Walimu na wakufunzi

 Kanal  Fabian Massawe akiongea na wanafunzi kuwapa moyo na kuwataka pale kwenye mapungufu waongeze bidii

 Mkuu akikagua maeneo mengine
 Choo kipya kimejengwa katika uwanja wa kaitaba
 Hii ndio Kufa KUFAANA
 kAITABA inavyoo vya kufrash utapenda
 Jukwaa maarufu kama Jukwaa la Balimi nalo linaezekwa
 Jamcobukoba.blogspot.com tunatoa pongezi kwa uongozi wa kitaifa na mkoa kwa kuleta uzinduzi huu katika mkoa wetu,chini ya kapeti ziko habari kuwa uwanja huu hivi karibuni utawekewa nyasi bandia,yote ni heri kwa wana Kagera, ukizingatia Rais wa TFF NI...... Malizia mwenywe, Wahaya wanasema Eofisi etainamu wawe eikala ekomile. asante WAJINA.