Thursday 27 February 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na

Wednesday 26 February 2014

Bi ASIMWE NGEMERA ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

 Bi Asimwe Ngemera akiwa na wanae wakisherekea siku yake ya kuzaliwa katika ukumbi wa Lina's
 Bi Asimwe (kulia) na swaiba wake Bi Anet wakiingia ukumbini
 Mwonekano wa eneo walilokaa
 Wajomba wa Asime Bw Mjuni Kataraiya na Bw Jafet Kataraiya
 Keki ikakatwa
 Karibu swaiba
 Naomba niwalishe watu wangu wa muhimu sana siku ya leo
 Shampein ikafunguliwa
 Ongera Asimwe kwa kufikisha miaka kadhaa
 Zawadi zikatolewa
 Msosi time
 Ukafunguliwa muziki
 Mjomba na mtoto uwanjani
 Kijana Kahabuka na chupa yake
 Wakati wa Muziki
 Kata kiuno mtoto wa kike kwa raha zako
 Mtu na mdogo  wake
Mc Baraka akimpongeza Bi Asimwe

MISAADA KWA YATIMA NA MAPACHA WANNE YAFIKA SALAMA MBEYA




Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.

Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique 
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
-----------------------
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.com) kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne  ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la  Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye  ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
 Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza  safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne. 
Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana. 
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
Nasi tutafikisha ubani wako. 
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.