Na Faustine Ruta, Bukoba
Mabingwa watetezi Bilele FC wameanza kwa kufungua Michuano hii ya Kagasheki Cup vibaya baada ya Kutandikwa bao 3-1 na Timu ya Rwamishenye Fc leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini. Bilele FC ndio walioanza kuifunga timu ya Rwamishenye katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza, Bao likifungwa na Miraji Ramadhan.
Timu ya Rwamishenye waliongeza bidii ili wasawazishe bao na katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza walisawazisha bao kupitia kwa mchezaji wake Khalid Seleman na kuongeza tena bao jingine katika dakika ya 42 kupitia kwa Yahaya Sadiq aliyekuwa amevaa jezi namba 7 mgongoni na kufanya 2-1 dhidi ya timu ya Bilele Fc yenye makazi yake Bukoba Mjini wakifaamika zaidi kwa jina la KM.0, hadi mapumziko Rwamishenye ndio walikuwa mbele ya bao 2-1.
Kipindi cha Pili dakika ya 56 walioshona tena bao jingine la mwisho kupitia kwa mchezaji wake matata Edwin Edo na kufanya kipute kumalizika kwa bao 3-1.
Kesho Mtanange unaendelea na utazikutanisha timu za Bakoba na Kashai, Mtanange utakao pigwa saa 10:00 jioni. Jumatatu kutakuwepo na mitanange 2 wa saa 8 na saa 10 jioni.
Wachezaji wa Rwamishenye Fc wakishangilia moja ya bao lao

Wachezaji wa timu ya Bilele Fc wakishangilia bao lao la dakika ya 5 lilifungwa na Miraji Ramadhan

Kikosi Cha Timu ya Rwamishenye kilichoanza

Kikosi cha Timu ya Bilele FC

Timu zikisalimiana

Waamuzi na Timu Kapteni timu zote mbili wakilianzisha

Waamuzi wa Mtanange huu

Kikosi cha Timu ya Rwamishenye uwanjani wakiomba kabla ya kipute kuanza muda mfupi

Mgeni Rasmi akisalimia timu ya Rwamishenye

Mgeni Rasmi akisalimia timu ya Bilele Fc ambao ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hili

Mgeni Rasmi akiteta jambo na Wachezaji Pande zote mbili

Mgeni Rasmi wa pili (kusho) akiteta jambo kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la KAGASHEKI CUP 2014, Mzee Abdul Sued, (kulia) ni Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii jioni.

Mbwembe nazo hazikosi kwenye hii Ligi......

Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi huu wa Mashindano ya Kombe la KAGASHEKI CUP 2014, Mzee Abdul Sued alianzia hapa kwa kufungua hii Ligi kwa kumfunga kipa moja wapo kati ya timu hizi mbili.

Mashabiki wakishangilia timu yao

kipute kikiendelea..kaitaba

Wachezaji wa Timu ya Bilele walivalia jezi zinazofanana na Mbeya City

Patashika za hapa na pale zikiendelea, kila mchezaji akitaka aupate mpira

Kila Mchezaji alikuwa na mwenzake wakubanana nae.

Hapa ukatizi ndugu yangu!

Mpira ukiendelea..

Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye wakicheza muziki baada ya kusawazisha

Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi huu wa Mashindano ya Kombe la KAGASHEKI CUP 2014, Mzee Abdul Sued, (kushoto) ni Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii wakifuatilia kwa Karibu.

Mashabiki ndio usiseme...walijaa uwanjani Kaitaba

MashabikiWaamuzi wakina Dada nao walikuwepo wakitazama wenzao wakiendesha mpira

Mchezaji wa Rwamishenye akishangilia bao lake la pili lililofungwa na Yahaya

Wachezaji wa Rwamishenye wakishangilia bao lao baada ya kuwanyuka Bilele Fc

Bango la Timu ya Bilele Fc likiwa mbele ya Mashaki wake! wakisema si..si..simnaona!!!!!

Mashabiki baada ya kukutana na Camera..wakajimwaga kivyao!!! Ligi ya Nyumbani!!
