Wednesday, 9 April 2014

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KAGERA KUWASILI KESHO 10-4-2014 ,AMBAE PIA NI RAIS WA TFF JAMAL MALINZI

 Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera(KRFA) Jamal Malinzi atawasili  siku ya Alhamis 10-4-2014 majira ya saa nne asubuhi katika uwanja wa ndege wa Bukoba.Kwa mujibu wa Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama amewataka na kuwaomba wapenzi wa soka mkoa wa kagera kujitokeza kwa wingi uwanja wa ndege kumpokea mwenyekiti wao kwani tangu achaguliwe kuwa Rais wa TFF alikuwa hajabahatika kurudi nyumbani,Bw Jamal Malinzi atakapokuwa mkoani atahudhulia kikao cha kamati tendaji ya KRFA na siku inayofuata utakuwepo mkutano mkuu wa KRFA.
 Bw Salumu Chama Katibu wa KRFA
 Bw Pelegrinius .A. Rutayuga mjumbe wa kamati tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF  na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu, nae yuko tayari Bukoba kuudhuria kikao cha kamati tendaji na mkutano mkuu wa KRFA
 Mmiliki wa Bukobasports.blog akiongea mawili matatu ya kimichezo na Bw Rutayuga
 Mmiliki wa jamcobukoba.blogspot.com akiwa na Bw Rutayuga ambae aliweza kuongelea mambo mengi ya kimechezo na kati ya mengi alisema ndoto yao kubwa ni kuweka mikakati popote Tanzania bila kujarieneo au mkoa mpira uchezwe,ukue na kupata vijana wenye uwezo wa kukuza soka la Tanzania ,kuachana na mazoea au ukariri wa fulani ndio anaweza wakati vipaji viko kila mahala Tanzania.


Kila rakheri katika mapambano ya kukuza soka Tanzania

Tuesday, 8 April 2014

HUYU NDIE ASKOFU ANAYEISHI MAISHA YA KIFALME HUKO ARUSHA TAZAMA PICHA MBALI MBALI HAPO CHINI


ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.

Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.

Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania. Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’. “Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha. “Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.



CHUO CHA UALIMU ERA KINACHOFUNGULIWA MWEZI WA SABA MWAKA HUU CHAANZA UANDIKISHAJI WANAFUNZI, KUWA NA URAFIKI NA GLOBAL CITIZENS NETWORK YA MAREKANI

 Hatimae uandikishaji wa wanafunzi katika chuo cha ualimu ERA kinachotarajia kuanza mwezi wa saba mwaka huu,Akiongea na mmiliki wa Blog hii ,Mwanzilishi wa chuo cha ERA kilichoko Bukoba Manispaa, kata ya Kitendaguro nje kidogo ya mji wa Bukoba Ndugu Paskazia Barongo amesema maandalizi yanaendelea vizuri na taratibu zote zinaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanafunzi wanaotarajia kuanza masomo mwezi wa saba mwaka huu.Amesema Ndugu Paskazia Barongo kuwa ni matarajio yao kuwa wamejipanga vizuri kutoa Elimu Bora ili waalimu watakaohitimu katika chuo cha ERA waweze kutoa elimu bora katika shule za msingi popote Tanzania kwa Weredi na ufasaha mkubwa,Pia ameeleza kuwa ile kuboresha mahusiano na  vyuo vingine ndani na nje ya nchi chuo chao kimeanzisha urafiki na  Global Citizens network walioko Minneapolis Marekani ili waweze kushirikiana katika maswala ya Elimu kwa wanafunzi wa ERA kwenda Marekani na wa Marekani kuja ERA. Ndugu Paskazia Barongo ameitaka jamii kwa ujumla kuleta watoto wao waliomaliza kidato cha nne  na hawakuweza kupata nafasi wajiunge na chuo cha ERA na watajikomboa wao binafsi na kuwa Walimu wa mfano katika kutoa elimu bora nchini Tanzania.
 Mama Ashura( Fundi cherehani) akimpima Unifomu mmoja wa wanafunzi anaetarajia kuanza masomo  chuoni mwezi wa saba mwaka huu
 Vipimo vya Unifomu
 Bi Paskazia Barongo akiongea na wanafunzi wanaotarajia kujiunga na chuo, wakisubiri kupima Unifomu chuoni hapo
 Bi Linda Stuart (kushoto) Mkurugenzi wa Global citizens network ya Marekani akiwa na Mkurugenzi wa Cosad Ndugu Smart Baitani anaeishi  Marekani
 Wanachuo watarajiwa wanaoanza masoma mwezi wa saba mwaka huu
 bI Paskazia Barongo akiwakaribisha wageni
 Mkuu wa  Chuo cha ERA  Bi Paulina Ngina Musau akieleza namna walivyojipanga kutoa Elimu katika chuo cha ERA
 Mmoja ya wanachuo wanaojiunga akitoa neno la shukrani kwa kuanzisha chuo
 Mwanachuo mtarajiwa akipongeza uongozi kwa wazo zuri la kuanzisha chuo cha ualimu
 Mzazi akinukuu vifungu vya Biblia na kusema chuo cha ERA ni mkombozi kwa watoto wao
 Wakipata kifungua kinywa
 Mtoto wa Bi Linda Stuart akipata chai
 Mkuu wa chuo akimtembeza kumuonyesha mazingira ya chuo na sehemu ya mabweni, katika chuo cha ERA Godoro na kitanda unavikuta chuoni ili kumpunguzia gharama mzazi
 Ni vitanda imara na salama
 Vyoo vizuri kwa afya ya wanachuo
 Mazingira ya kupendeza
 Bi Paskazia akitoa maelezo
 Picha ya pamoja
Mkuu wa chuo Bi Paulina akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa chuo ambae pia ni mwalimu katika chuo cha ERA Bw Ocham Collins wakiwa na mtoto wao