HUYU NDIE ASKOFU ANAYEISHI MAISHA YA KIFALME HUKO ARUSHA TAZAMA PICHA MBALI MBALI HAPO CHINI
ASKOFU
na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry
‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni
alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi kwa kuwa na magari ya kifahari
na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga
kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wakutosha.
Katika
mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu
alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa
njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali
ambao haujawahi kutokea.
Mbali
ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi
karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa
yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma
katika makanisa ya kiroho Tanzania. Akiwa Karatu, mbali na ulinzi
binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi,
askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa
usalama barabarani.Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa
wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na
askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi
wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete ‘JK’. “Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini
mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii
ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda
kutajwa gazetini.
Hata
hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana
na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu
mbalimbali jijini Arusha. “Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi
fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja
la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia
kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.
No comments:
Post a Comment