Friday, 7 June 2013

WAKATI WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAKIJIANDAA KUELEKEA KATIKA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI MH MBUGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI KAGASHEKI ATOA SWADAKA YA MISWALA KWA MISIKITI YOTE JIMBONI KWAKE




mh mbunge wa jimbo la bukoba mjini ametoa swadaka ya miswala katika misikiti yote katika jimbo lake  mh kagasheki katoa miswala hiyo kwa kutambua mahitaji makubwa ya miswala katika misikiti hiyo ili iweze kusaidia waumini wakati wa ibada,mapema mwezi wa saba waumini wa kiislamu duniani wataanza mfungo wa ramadhani,kwa hiyo ni imani ya mbunge kuwa kipindi hicho waumini wengi ufanya ibada zao ,hivyo miswala hii itasaidia.


                                 baadhi ya miswala ikiwa kwenye gari ikisambazwa  maeneo  tofauti


                                     msikiti wa kibuye kwa haji hamza

 kulia ashirafu kalumuna,ramadhani kambuga na haji hamza wakiwa maeneo ya msikiti wa kibuye,muda mchache kabla ya ujumbe kutoka ofisi ya mbunge kukabidhi miswala













                                                 miswala ikitandikwa















                             eneo la kiwanda cha kahawa cha amir hamza maeneo ya kibuye








                                               ni kupakua kwenye gari na kuweka msikitini






                                    ni msikiti wa kagondo



                                                   mmoja wapo ya miswala





                                                                            ni furaha tupu


                             ni zoezi la kutandika miswala kila msikiti jimbo la bukoba mjini






 mwenyezi mungu amzidishie balozi kagasheki,ni dua zilizotawala maeneo yote ya misikiti waliopokea miswala



                                             akina mama wakifurahia

















alhaji katema akishukuru uongozi kutoka ofisi ya mbunge kwa kuleta miswala msikiti wa kashenye kashai




 ni msikiti  ulioko maeneo ya mwalo wa kifungwa,msikiti huu hutumiwa na wavuvi wa eneo hilo


                               ni maeneo ya mwalo wa kifungwa ziwani noko walipata miswala











                                           msikiti ukiwa tayari umeshatandikwa miswala


                                               amina....,amina.... amina.....





waumini wa msikiti wa nyaishenye sekondari wa kiomba dua ya kushukuru na kumuombea mh kagasheki kwa kuwaletea miswala








                                   miswala ikitandikwa  katika moja wapo ya msikiti iliyopata miswala




                                          miswala akishushwa msikiti wa jafaries
mwenyekiti wa msikiti wa jafaries murtaza visram akipokea miswala kwa ajili ya waumini  wa msikiti wake,anaonekana akimsikiliza ashiraf kalumuna aliekabidhi miswala hiyo kwa niaba ya  ofisi ya mbunge jimbo la bukoba mjini

REDD'S MISS MARA 2013 YAPEWA MIL. 10 KUTOKA AFRICA BARIC GOLD

Ofisa kutoka kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barrick Gold Mining Fatuma Mssumi akimkabidhi Kaimu Ofisa Tawala wa Mkoa wa Mara mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo kwenye mashindano la Redd's Miss Mara yatakayofanyika leo mjini Musoma.Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd's Miss Mara 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jana ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.
Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Mara 2013 wakiwa wenye furaha.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd's Miss Mara 2013 wakitembea kwa pamoja leo ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

YANGA NAYO KUTOENDA DARFUR KUTETEA KOMBE LAKE

Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo cha karibu na uongozi wa klabu wa Yanga ni kwamba mabingwa hao watetezi wa kombe la Kagame hawatoenda kushiriki michuano hiyo mwaka huu iliyopangwa kuanza hivi karibuni huko Darfur Sudan.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya serikali kupitia wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kusema kwamba haioni busara kwa vilabu kwenda Darfur kwa sababu eneo hilo bado halina usalama wa kutosha - kauli iliyopelekea mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage kusema kwamba timu yake haitokwenda Darfur kushiriki michuano hiyo mwaka huu.

Kwa mujibu wa CECAFA na chama cha soka cha Sudan ni kwamba michuano hiyo itachezwa kwenye lililo salama na lenye ulinzi mkubwa hivyo timu hazihitaji kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao pindi watakapoenda kushiriki michuano hiyo mapema mwezi ujao.

Hatua ya Yanga kujitoa inazidi kuongeza idadi ya vilabu ambavyo vimesema ikiwa michuano hiyo itafanyika Darfur basi havitashiriki Kagame Cup mwaka huu, vilabu vikubwa vya Sudan AL Hila na El Merreikh, Tusker ya Kenya na Simba SC vyenyewe vilishatangaza uamuzi wa kutokwenda Darfur kwa ajili ya michuano hiyo.

Thursday, 6 June 2013

WALIO KAMATWA NA UNGA EGYPT NI WATANZANIA WAWILI NA UWEZEKANO WA KUNYONGWA NI MKUBWA.

Pichani ni mmoja wapo wa wasichana walio kamatwa nchini Misiri akiwa na unga unao semekana ni hereoin. Bado hatuja weza kupata details za mthumiwa wa pili.

Dar es Salaam. 
Watanzania wawili wanashikiliwa nchini Misri baada ya kukamatwa wakiwa na kilo saba za dawa za kulevya aina ya heroin wiki mbili zilizopita walizokuwa wameficha kwenye begi la nguo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mkubwa Ali, alikiri kukamatwa kwa watu hao (majina yanahifadhiwa) ambao mmoja ni mkazi wa Ilala na mwingine wa Magomeni jijini Dar es Salaam. “Taarifa tulizonazo zilizo rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa sasa ni kukamatwa kwa Watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha heroin kuelekea Bara la Asia na walikamatwa nchini Misri wiki mbili zilizopita.”

“Tumewasiliana na balozi wetu nchini Misri amesema hana taarifa za kuhukumiwa kunyongwa kwa watuhumiwa hao, isipokuwa wameshasomewa shtaka lao la awali. Wapo rumande kwa sasa kwani kesi hiyo imetajwa mara moja tu. Balozi amekiri kushikiliwa kwa watuhumiwa hao wakiwa na dawa zinazoaminiwa ni za kulevya,” alisema.

Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa polisi na wanatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Video inayomwonyesha mmoja akikaguliwa na maofisa wa polisi wa nchini Misri na kukutwa na dawa hizo, ilisambaa siku nne zilizopita katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa mujibu wa sheria za Misri kama ilivyo kwa nchi za Bara la Asia, mtu akikamatwa na dawa za kulevya hukumu yake ni kunyongwa hadi kufa. Kutokana na sheria za nchi hiyo, tangu kukamatwa na Watanzania habari zimeenea kuwa huenda wakanyongwa.

Habari za uhakika kutoka kwa ndugu wa karibu wa mtuhumiwa huyo, zilidai kuwa walikuwa hawafahamu kuwa alikuwa anajihusisha na dawa za kulevya.

“Huyu ni ndugu yangu kabisa lakini nilikuwa sijui kama anafanya mambo kama hayo’’ alisema.

Kama atanyongwa ni pigo kubwa kwetu,” alisema mmoja wa ndugu wa Sharifa ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Alisema miaka mitatu iliyopita ndugu yao wa kike mwenye mtoto mmoja alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Nivea na alikuwa hana tabia mbaya.
Mthumiwa mmoja wapo akiwa na mwanae wa kike
Jana mwandishi wa habari hizi alilifika katika Ubalozi wa Misri nchini ili kufahamu kwa kina habari hizo, ambapo balozi wa nchi hiyo hakuweza kuzungumzia lolote.

Hapa chini kuna link ambayo iko uptodate inforamtion ya adhabu ambazo wathumiwa mbali mbali hupata nchini Egypt baada ya kuhukumiwa na case tofauti ikiwemo madawa ya kulevya bofya ujisomee.

Death Penalty WorldWide

Wednesday, 5 June 2013

ULINZI WAHIMARISHWA NYUMBANI KWA MAMA YAKE NGWEA NA MOROGORO YOTE, CHEKI PICHA WAZEE WA KAZI WAKIWA MZIGONI


WAKAZI WA MANISPAA YA MOROGORO NA VITONGJI VYAKE WAKITAKA KUSUKUMA GARI LILILOBEBA JENEZA LENYE MWILI WA ALBERT MANGWEA MARA BAADA YA KUTOLEWA NDANI KWA MAMA YAKE MANGWEA KIHONDA MOROGORO LAKINI NAFASI HIYO HAWAKUWEZA KUIPATA NA KULAZIMIKA DEREVA WA GARI HILO KUONGEZA MWENDO HUKU LIKIONGOZWA NA KING'ORA CHA JESHI LA POLISI KUELEKEA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI MAJIRA YA SAA 1:45 USIKU HUU. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI WILAYA YA MOROGORO ABDALLAH HUSSEIN KULIA AKIWAPA MAELEKEZO ASKARI ILI WAWASOGEZE WANANCHI ILI IPATIKANE NAFASI YA KUTOA JENEZA LENYE MWILI WA MANGWEA UKAHIFADHIWE CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO.ASKARI KANZU AKIWA KWENYE LINDO MARA BAADA YA JESHI LA POLISI KUONGEZA ASKARI KWA AJILI YA ULINZI NYUMBANI KWA MAMA YAKE MANGWEA KIHONDA MARA BAADA YA KUWASILI KWA MWILI WA MANGWEA MAJIRA YA SAA 12 JIONI ASKARI AKIWA AMEOKOTA KANDAMBILI NA KUZINADI KWA MWENYEWE BAADA YA KUWASOGEZA WATU AMBAO WALIZIBA SEHEMU YA MLANGO WAKATI WAKITAKA KUONA JENEZA LENYE MWILI WA MANGWEA WAKATI LIKTOLEWA NDANI NA KWENDA KATIKA CHUMBA CHA MAITI CHA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO.HAWA NI WALINZI KUTOKA DAR AMBAO WAPO KATIKA KAMATI YA MAZISHI YA MAREHEMU MANGWEA WAKIWA WAMEKAA MLANGONI WAKATI JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA NYUMBANI KWA MAMA YAKE KIHONDA MOROGORO BAADA YA KUWASILI KUTOKA DAR ES SALAAM MAJIRA YA SAA 12 JIONIASKARI WAKIWATWANGA MASWALI KWANINI MMEPANDA JUU ?, JIBU ILIKUWA JEPESI TU, TUNATAKA KUONA JENEZA LA MANGWEA MSHKAJI WETU.P-FUNK a.k.a MAJANI KULIA NA AFANDE SELE (SELEMAN MSINDI) MUDA MFUPI BAADA YA MWILI KUWASILI KIHONDA MOROGORO.HUYO NDO KITALE ? ANAWAPA HI WASHKAJI MARA BAADA YA KUWASILI KWA MWILI WA MANGWEA NYUMBANI KWAO KIHONDA MOROGORO SAA 12 JIONI.